Kwa wale wote wenye nia njema na Tanzania hawawezi kumpigia kura Mh Slaa. Kumpigia kura Mh Slaa ni sawa na kuitosa Tanzania katikati Bahari.
Ukidhani uchaguzi ni Mchezo, basi unapotea. Na mwenye kubeba mzigo sio Viongozi waliopo madarakani sasa hivi bali ni wewe mpiga kura - mlala hoi.
Ukitaka kujua hatari ya huyu mtu angalia marafiki zake wa karibu na wale wanaosimama majukwaani na kusema "msichague chama, chagueni mtu". Huu ni ujinga kabisa, kwani hii ni nchi ya kidikiteta? Hivi ni mtu mmoja atayeiongoza hii nchi au ni ilani ya chama?
Katika nchi yeyote ile inayofuata demokrasia, Rais hana nguvu ya namna hiyo. Na hapa ndio utajua ajenda za siri na makubaliano yaliyokuwepo kati ya Mh Slaa na hao watu.
Tatizo kubwa la huyu Mh ni elimu aliyosoma, apende asipende inamsogeza karibu na udikiteta. Sasa tulimkataa DIKITETA Idd Amini, baada ya miaka kadhaa tunamchagua Dikiteta Slaa. Kwa taarifa yenu dikiteta wa kuchaguliwa ni hatari zaidi kuliko yule aliyeingia kwa kupindua nchi.
Nchi itagawanyika vibaya sana ikiwa ndoto yake itakamilika.
Kuwa Mh Slaa ni Dikiteta nilishayaona wakati nilipokuwa CHADEMA. Sasa nimeamua kuwaelezeni ili mumfahamu Mh Slaa ni nani? Unachoweza kukifanya ni kutompigia kura huyu Mh.
Unaipenda Tanzani? Msikilize tu Mh Slaa lakini kura yako mpe Kikwete.