Ndio siku zimekaribie, lakini moja la muhimu ni hapo uliposema:
"Au mwekeni fisimaji mmoja agombee uraisi uone kama atapata"
Ndugu yangu Chama ni 'trade mark' muhimu sana. CCM ilipomuweka MKAPA kugombea watanzania wote hawakumjua utendaji kazi wake wala hakuwa hata katika 10 bora waliojulikana (CCM) na watanzania. Hata 3 bora kwa wagombea wa upinzani. Watanzania walichofanya walichagua chama kwa vile walijua hata kama atateteleka basi wapo magwiji watamuonya hata pengine kutompa kipindi cha pili. Isitoshe ILANI YA UCHAGUZI ILIKUWEPO TAYARI, NA SI YEYE ALIYETENGENEZA. Hivyo alichotakiwa ni kufuata RELI tu na si vinginevyo.
Sasa wenzetu mnakotaka kutupeleka ni kule ambako Tanzania haipaswi kupita. Kuwa mtu (Rais) aendeshe utawala wa kidikiteta, asisikilize ILANI bali aendeshe kutokana na kichwa chake mwenyewe. Hivi nyie mnaelewa hatari ya haya maneno. Hivi mnajua ni asilimia ngapi ya wabunge wakitia kura za 'NDIO' ili kupitisha elimu bure. Atapata hiyo idadi ya wabunge? Hapa ndipo mtataka atumie mabavu. Na kwa kufanya hivyo ndio mwisho wa amani.
Jamani msicheze na watanzania mkidhani mtawaburuta mtakavyo nao kwa jina la amani watakaa kimya tu. Anayefikiri hivi anajidanganya. Ombeni radhi ili mjisafishe.