Kama unajiita maskini jeuri, jua hiyo jeuri ndiyo inafanya uzidi kuwa maskini

Kama unajiita maskini jeuri, jua hiyo jeuri ndiyo inafanya uzidi kuwa maskini

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Mara kadhaa Masikini tumekuwa na kauli mbali mbali za kuonyesha kuwa Umaskini ni haki yetu na moja wapo wa kauli ni hii MASKINI JEURI, Yaani Maskini pia Jeuri .


Na kweli ukiwaona MASKINI jeuri utasema kweli jeuri imewaponza , Kwa sababu wamejiweka kwenye mazingira ambayo hawasaidiki

Maskini jeuri utakuta wana sifa hizi:
1.Kuwasema vibaya matajiri kutwa nzima.
2.Kuwachukia matajiri bila hata sababu zenye mashiko.
3.Kujifanya wajuaji sana na ubishi kupitiliza.
4.Kujitenga na matajiri kwa dhana ya kutojipendekeza kumbe ndio wanajikandamiza.
5.Kujisia kwa jeuri zao za kimaskini.


Sina maana ujipendekeze kwa matajiri ila namaanisha usijipe jeuri inayofanya utengwe , muda mwingine fursa hutoka kwa watu sasa kwa jeuri yako hiyo utaendelea kubaki kwenye umaskini huo maisha yote.

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto Zako.
 
Umegusa mule mule na tabia hyo kuna watu weng humu JF wanayo, wao kila tajir kwao ni utajir wa mashart au fisadi
 
Back
Top Bottom