Kama unamiliki kitambulisho cha NIDA utakubaliana na mimi kwenye mambo yafuatayo

Kama unamiliki kitambulisho cha NIDA utakubaliana na mimi kwenye mambo yafuatayo

Tesco Tesco

Member
Joined
Jun 3, 2024
Posts
7
Reaction score
20
Nafikir kama unaimiliki namba ya Nida au kitambulisho Cha NIDA hasa wale walioandikishwa wakati zoezi la utoaji wa NIDA linaanza utakubaliana na mimi mambo yafuatayo:

1.picha zetu sio halisia
2.kadi Zina makosa mengi Kama
A .majina yamekosewa Sana
B.Tarehe za kuzaliwa zimekosewa pia

Ningeshauri kuwen na mda wa kuhuisha taarifa zetu ili vitambulisho vyetu viwe na uhalisia kwani vinatupa shida kwenye matumizi mbalimbali..Asante🙏
 
Ufanye uzembe wewe uwasingizie nida .......mbona kitambulisho changu hakijakosewa na pia pale anapoingiza taarifa zako yule mfanya kazi lazima akugeuzie computer uhakikishe taarifa kama ziko sahihi.
 
Vitambulisho havina ubora, taarifa zinafutika haraka mno.

Kadi yangu nimeenda kuichukua tayari baadhi ya taarifa zimekwishakwanguka kwa ule msiguano wa kadi nyingine pale ofisini.
 
sasa mimi nimeomba wanirekebishie jina langu tangu mwaka jana 2023 April hadi hii 2024 Octoba, wananiomba cheti cha ubatizo na vyeti vya kuzaliwa watoto???, vyeti vyangu vyote niliwapa wakasema ongezea na cha ubatizo...hakuna majibu. Siku nimewapelekea yule aliyevipokea anashangaa eti kwani tulisema cheti cha ubatizo nacho...nikawapa barua waliyonitaka niwape nikaona macho yanawatoka...nawa zoom tu!!!. wa hovyo sana hao nida, wamepeana ajira kwa ngono na undugu tu humo maofisini..hakuna weledi wowote yaani
 
Mmi ni miongoni mwa walioandikisha wakati zoezi ndio linaanza. Picha na majina hakuna kilichokosewa
 
MImi pia wale wa mwanzo ambao vitambulisho havina sahihi lakini ni bora na havikukosewa majina
 
Ufanye uzembe wewe uwasingizie nida .......mbona kitambulisho changu hakijakosewa na pia pale anapoingiza taarifa zako yule mfanya kazi lazima akugeuzie computer uhakikishe taarifa kama ziko sahihi.
hakuna ulazima wa ku criticise kama kwako iko vzr
 
🤣🤣 ni mfumo tu.
Sisi tunakula keki ya taifa tena kwa kujikatia li-kipande vitambulisho vyetu ni OG
 
Ufanye uzembe wewe uwasingizie nida .......mbona kitambulisho changu hakijakosewa na pia pale anapoingiza taarifa zako yule mfanya kazi lazima akugeuzie computer uhakikishe taarifa kama ziko sahihi.
Hamkosekanagi.
 
Back
Top Bottom