Kama unamuamini Mungu mshike kweli kweli na kama unaloga loga kweli kweli binadamu wabaya

Kama unamuamini Mungu mshike kweli kweli na kama unaloga loga kweli kweli binadamu wabaya

Expensive life

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2020
Posts
2,971
Reaction score
9,437
Ndugu zangu, jana nilienda sehemu kumsalimia shangazi yangu, sasa baada ya kufika pale nimemkuta mume wake akiwa kitandani amepooza hawezi kabisa kutembea ni miaka mitano sasa imepita toka awe ndani.

Kifupi nina muda mrefu sana sijamuona mumewe japo hili tatizo alilonalo nilisha lisikia muda.

Wakati napiga stori na huyu mume wa shangazi, kaniadithia mengi sana mazito, alikuwa ni mtafutaji mzuri sana alikuwa na marafiki wengi sana majumba magari alikuwa nayo.

Ulikuwa ukienda pale nyumbani kwake utakuta watu wa kila aina kiufupi alikuwa ni mtu wa watu, tatizo lilimuanza mwaka 2018 kama masihara tu akiwa kwenye harusi ya ndugu yake ghafta tu akiangua.

Hivyo kuzusha taharuki kubwa pale ukumbini, karatibu zilifanyika haraka kumuwahisha hospitalini.

Baada ya kumfikisha hospitali na kisha kufanyiwa vipimo daktari alidai kuwa persha yake ipi juu sana, hivyo wakaanza matibabu haraka huku mgonjwa akiwa hajitambui kabisa ( mahututi).

Week imepita hajitambui kabisa, ndugu nao wakakata tamaa ikabidi waanza kujadili ni wapi tutamzika huyu ndugu yetu maana kwa hali aliyokuwa nayo hawezi kabisa kupona.

Mungu ana maajabu yake kwa bahati nzuri mgonjwa akafanikiwa japo kufungua macho.

Hapo ule mkakati tutamzika wapi ukafa, taratibu mgonjwa akaanza kurikava, baada ya kama mwezi hivi akarudi kwenye hali yake ya kawaida ila akawa hawezi kuzungumza chochote wala kutembea.

Taratibu za kumrudisha nyumbani zikafanyika, watu wakasema hii siyo hali ya kawaida hapa inabidi tutembee watu wakatembea, hivi sasa anazungumza vizuri tu ila kilichobaki ni kutembea.

Bado watu wanaimani ataembea tu.
 
Unaweza ukasema mtu ana pesa, magari, majumba, bila ya kujua dhahama za madeni mbalimbali anazokabiliana nazo. Hayo hayampi mtu Amani, na ukizingatia haya wenye uwezo hawana mazoea ya kuangalia afya zao, basi majanga kama haya ni lazima yatatokea. Si uchawi, ni hali halisi ya kibinadamu.
 
Back
Top Bottom