Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Kama mahusiano yako yanakufanya ujisikie kuchoka na hauna raha,basi si wakati muafaka kwako kuendelea nayo
Kama unajikuta kila unachofanya ni kwa ajili ya kuhakikisha mahusiano yako yanaendelea basi jua unapoteza namna ya kufanya mambo yako mengine,kwa maana nyingine umepoteza uhuru wa kufanya mambo yako.
Kama pamoja na kuwa katika mahusiano lakini bado unajisikia upo mpweke basi huo uhusiano hauna afya nzur sana kwako,ni bora kufikiria namna nyingine ya kufanya.
Ikiwa katika mahusiano yako ugomvi huwa mwingi zaidi kuliko amani basi jua hapo kuna shida mahala,kuna mahusiano mengine ugomvi ndio sehemu ya kila siku basi tambua hapo utakuwa chizi wa mapenzi mda si mrefu.
Endapo mahusiano yako yanakufanya ushindwe kufanya baadhi ya mambo ambayo ni muhimu kwako na yenye thamani kwa kile kinachoitwa uchague mambo yako au mapenzi,hapo umepigwa,angalia namna nyingine
Ikiwa mahusiano yako hayakufanyi uwe mtu bora na mwenye mabadiliko hapo kuna shida,sio katika mtazamo wa kiuchumi laa! Ila katika namna nzima ya kuishi maisha yako
Na mwisho kama unakaa kwenye mahusiano kwasababu ya kuogopa upweke tu na si kufurahia mapenzi hapo pana shida,jiongeze
Ni hayo tu!