Kama unapenda kucheza Draft huna haja ya kushinda kijiweni tena

Kama unapenda kucheza Draft huna haja ya kushinda kijiweni tena

Hiyo ni sawa na kucheki UEFA au Ligi kubwa Ulaya ukiwa Sebuleni na Mke wako,haileti msisimko.....
 
raha ya draft sio kusukumiza kete ni zile kauli za shombo za wazee
ndo maana kuna wengne hata hawachez wao wanapiga story tu pale
 
hili draft ni rahisi sana, nimecheza iyo spanish ndo watanzania wengi tunaicheza, nimefika mpaka mpaka Grand master nikampiga mabao 10, ata droo hajatoa. kama lipo jengine lete ila sio hili. hili lina bibonde asa, kazi yao kuumiza kucha tu
 
Kabla ya kupata jibu jiulize kazini simu mzima au mnaacha wazi??
Ukiwa mfanya kazi wangu, kisha unaenda kucheza draft kazini au game ya aina yeyote nakutimua, inaonekana hauta kuwa na inovation yeyote kwenye kazi yako
 
768d40ed8c6667343a4fac8d074de31b.jpg


Unapenda au unajua kucheza Draft? Siku hizi vujiwe vya kucheza vimepungua sana, kwanini...?
Kumbe wazee vijana na watu wote wanashinda kwenye simu zao.
Sasa unaweza kucheza kwenye simu yako, angalia na kupakua usisahau kumpakulia mzee wako mwenye simu janja yake ili achezee popote, apunguze kwenda kijiweni unaweza kuangalia toleo kama la Tanzania na kupakua hapa Cheza Draft la Tanzania kwenye Simu yako sasa ~ SmatSkills
Hilo Mi ndo nacheza now mwaka umeisha,nilikuwa sijui but nilipozoea nikaenda kucheza mtaani nikawa nawafunga sana
 
Draft la kijiweni bhana? Enzi hizo napiga kete jiwe na kujishindia bonge la jogoo..
 
Back
Top Bottom