Mbeya kukaa mtaani ni ahueni zaidi kuliko hiyo 240,000/= kwa sababu hostel utalazimika kunjinunulia chakula. Hostel zao zenyewe sio nzuri ni kama dizaini ya Mabweni fulani hivi. Ukipata nyumba/Chumba chako maeneo ya Soweto (gharama kidogo kubwa kwa sababu ni karibu na Chuo), Ilomba, Sae na Mwanjelwa ni maeneo ambayo hutalazimika kupanda gari kwani unatembea na maisha yapo chini sana. Ukitaka kupanda gari walau kwa shilingi 300 kwenda na kurudi unaweza kuishi hata Nane Nane, Uyole, Mafiati, Airport, Soko Matola n.k
Kiufupi Mjin wa Mbeya ni mzuri sana kwa mtu mwenye maisha ya kawaida kama Mwanafunzi wa Chuo, ukipata mkopo utaishi bila shida yoyote. ONYO: Maeneo ya starehe kama vile Mbeya Carnival, Shaba Pub, Nebana na Pamodz ni hatari sana utafilisika (Utani!) .
Nondo pia zinatembea nje nje na mwaka jana tulizika Mwana Chuo wa TEKU
Vinginevyo Karibu sana Mbeya