Kama unatafuta nyumba ya kupanga DSM, kuna vitu vya kuzingatia usivichukulie poa!

Namba 3 linaenda kunikuta aiseeπŸ˜“ ila baba huyu anaonekana mwaminifu sana
Utalia na kusaga meno. Mi nilihisi ivo ivo

1. Hamna aluminum hadi leo, mwezi wa 2 na nusu.

2. Bafuni hamna shower hadi leo.

3. Jikoni hamna sinki na makabati as promised, na tiles bado nusu.

4. Feni ya juu hamna bado.

Usipokua mkali, iyo hela anaila hafu ndio nitolee.
 
Vyote vya Nini Ivo,mie amalizie kuweka vioo madirishani niingieπŸ₯΄
 
Pole mkuu.
 
Point ya Kuongeza ,Kama uchumi unaruhusu jitahidi ukae chumba chenye choo ndani kuna watu ni wachafu duniani na hawajali ,kuna muda unaogopa kuleta hata mgeni nyumbani Kwako
Dah muhimu sana.

Kuna nyumba nilikaa, choo cha kushare. Kuna mwamba alikua akiingia, ata kama kina maji yeye anashusha mzigo bila kumwaga maji.

Yaani ukiingia unaukuta mzigo pale, wakati maji sio kwamba hayapo.
 
Jenga ya kwako hata Chumba kimoja hii itakuweka huru
Kuna watu hawataki kuacha alama ya kujenga nyumba hapa duniani. Nina rafiki mkaka, angeweza kujenga hata nyumba 3 ikiwemo ghorofa.
Ila hataki kusikia neno kujenga! Yeye anapanga nyumba nzuri za bei sehemu nzuri. Akichoka anakaa hotelini ndiyo maisha yake mwenyewe kayachagua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…