Kama unatafuta nyumba ya kupanga DSM, kuna vitu vya kuzingatia usivichukulie poa!

Wenye nyumba hawanaga mtetezi.. Tatizo Wapangaji wengi wanajiandaaga kushindwa kukaa na mwenye nyumba kabla hawaja kaa nae, matokeo yake kila ikitojea wanapishana basi ina onekana kisa ni mwenye nyumba.

Mkataba ndio kila kitu iwe una kaa na mwenye nyumba ama na wapangaji wengine wengi.. hakikisha unaishi ndani ya mkataba wako na mwenye nyumba na usivumilie unapokiukwa.

Wengi wetu ni waoga katika kutetea haki zetu ndio maana tuna kua wanyonge hadi kwa Mali za watu tunazozitumia kwa kuzilipia. Ujue unapopanga mlinzi wako ni mkataba.

KWAKIFUPI.
Mimi ni mwenye nyumba na wapangaji wangu wote waliopita kwangu tumejikuta ni marafiki wakubwa na kama ndugu. Ninachowaambia mimi ni Jirani yenu, U Mwenye nyumba tutakutanishwa na mkataba. Na ninaishi nao nyumba moja tukishare makorido bila nyodo wala unyonge.

Kikubwa, Usijiandae kushindwa kuishi na mwenye nyumba.. tengeneza au kubaliana na mkataba utakaokufanya uishi maisha yako hata kama unaishi na mwenye nyumba bila karaha.
 
Changamoto mojawapo kubwa kukaa na mwenye nyumba, halafu awe ni mwanamke au mzee fulani mswahili! Utafurahi mbona!!
Hakuna raha kama ya kuishi na mwenye nyumba.. Unachotakiwa usimuogope tena mchukulie kama jirani na alijue hilo yaani hata akikuletea za umwenye nyumba wewe mwambie unamtambua kama jirani ila mkataba ndio unamtambua yeye ni mwenye nyumba. na ni kipengele gani cha mkataba kimekiukwa kama hakipo ishi maisha yako fresh kabisa.

Unajua mwenye nyumba akikusumbua ukimfungia kazi anatakiwa yeye ndio akutafutie pakukaa na ni pale utakapopapenda wewe mwenyewe?
 
Wanaboa kichizi, bado nikanunua submeter mbili za umeme laki 2 na sabini afu anasema hii pesa hatuweki kwenye miezi Sita uliyolipa ila tutaweka miezi Sita ya mbeleni utakayolipa, shikamoo wenye nyumba, Yan kama si utulivu wa huu mtaa na ningeshafanya maamuzi magumu
Mi miezi 6 ikiisha nasepa simpi 2nd chance
 
Nilipokaa mwanzo ukifika ule mtaa mchana unaweza Lipa kodi ya miaka miwili ila ikifika jioni hata ukiwa unaongea na mtu ndani anaweza akuambie ingia ndani tuweze kusikilizana iilhaali wewe upo ndani, kelele za pale si mchezo
Hahaha Dar sio ya kufanya maamuzi mchana au kiangazi. Utalia
 
Wenye nyumba hawanaga mtetezi.. Tatizo Wapangaji wengi wanajiandaaga kushindwa kukaa na mwenye nyumba kabla hawaja kaa nae, matokeo yake kila ikitojea wanapishana basi ina onekana kisa ni mwenye nyumba.

Mkataba ndio kila kitu iwe una kaa na mwenye nyumba ama na wapangaji wengine wengi.. hakikisha unaishi ndani ya mkataba wako na mwenye nyumba na usivumilie unapokiukwa.

Wengi wetu ni waoga katika kutetea haki zetu ndio maana tuna kua wanyonge hadi kwa Mali za watu tunazozitumia kwa kuzilipia. Ujue unapopanga mlinzi wako ni mkataba.

KWAKIFUPI.
Mimi ni mwenye nyumba na wapangaji wangu wote waliopita kwangu tumejikuta ni marafiki wakubwa na kama ndugu. Ninachowaambia mimi ni Jirani yenu, U Mwenye nyumba tutakutanishwa na mkataba. Na ninaishi nao nyumba moja tukishare makorido bila nyodo wala unyonge.

Kikubwa, Usijiandae kushindwa kuishi na mwenye nyumba.. tengeneza au kubaliana na mkataba utakaokufanya uishi maisha yako hata kama unaishi na mwenye nyumba bila karaha.
At least wewe unajua unachofanya. Na unaichukulia serious iyo "kazi" .

Hawa wengine wanaona kama wanatusaidia sisi hatuna pa kukaa.
 
Kama
Nilikua kwenye nyumba ya kupanga, nzuri tu. Tatizo mwenye nyumba akapandisha bei kwa asilimia zaidi ya 25, bila taarifa mapema.

Nikaona sio shida, nikahama mkataba ulivyoisha. Sasa katika harakati za kutafuta nyumba, kuna vitu nimejifunza na vingine nimeshachelewa nimejikuta najuta tayari niko ndani.

Baadhi yake:

1. Usikae na mwenye nyumba.

Nilipokua zamani nilikua sikai na mwenye nyumba. Anakuja mara chache sana. Ila sahivi nimeyatimba.

Hafu mwenye nyumba ana shughuli kila siku, mazingira yapo ovyo wala sio masafi kwasababu yeye tu ana ndugu zaidi ya 8 na watoto, ukijumlisha mnashare uwanja, aisee.

2. Jitahidi msiwe mna-share bili/matumizi ya maji au umeme.

Iwe na wapangaji wenzako au mwenye nyumba, jitahidi sana ulipie bili mwenyewe.

Ikitokea umebanwa sana bdsi angalau muwe wawili mwisho. Sub-meater hazitasaidia kitu. Mtatoa kila mtu 20,000/= ya umeme kwa mwezi wewe unashinda kazini ukirudi unawasha feni tu, kuna sista duu anachemsha maharage kwa presha cooker.

Lazima mtagombana tu.

3. Hakikisha nyumba imekamilika ujenzi, asikudanganye lipia tu namalizia wiki ili kuweka madirisha sijui.

Unavyoenda kukagua eti nyumba haijakamilika choo au dirisha, akasema lipia namalizia mtego huo.

Ukishalipia tu imeisha. Utakuta jikoni hakuna sink, feni ya sebuleni haweki, na ata maji unaweza kuta akachelewa kuyaingiza.

Jitahidi uende nyumba iliokamilika kila kitu.

4. Kama una gari, angalia upatikanaji wa funguo za geti.

Otherwise utajikuta unawahi kurudi kuogopa kufungiwa geti kama mtoto. Zamani nilikua ata saa 8 usiku naweza kutoka sahivi nawahi home saa 4 wasije funga geti. Nishalalamika ila ndio ivo, kila siku ahadi hewa.

5. Zingatia idadi ya wapangaji wenzako.
Kama unaweza, jitahidi wapangaji muwe wachache. Mkiwa kikosi kuna faida na challenge zake. Faida moja wapo unaweza pata mke hapo hapo. Ila hasara unakuta challenge hadi kwenye kamba za kuanika mfano weekend mkifua wengi kwa pamoja, makelele kila mtu akiweka singeli nk.

6. Uliza kuhusu utaratibu wa bili za maji taka, takataka/usafi na ulinzi shirikishi.

Hii michango haiwagi mikubwa ila nayo ni kero.
Kuna hii ya maji taka kuyatoa kwasababu shimo limejaa, michango ya wale wazoa takataka na ulinxi shirikishi.

7. Zingatia msimu wa mvua kunapitika? Mafuriko na nyumba kuvuja?

Kuna nyumba msimu wa mvua hazifikiki sio kwa gari wala kutembea, pia kuna uwezekano mvua ikinyesha nyumba ikawa inavuja.

8. Kelele/mishemishe za majirani.

Unaweza ukawa umeenda kucheki nyumba ukakuta pako cool, kumbe jioni kuna bar uchwara inapiga music usiku kucha.

Au ukakuta weekend au jioni ni nyumba za ibada wanatumia maspika ww unasema unapumzika wao wakakiwasha.

Kwa sasa nimeyatimba, ila kutaka kuforce kukaa Makongo Juu kumeniponza. Nikimaliza Kodi yangu naamsha.
Bachela uwe na box la condom usisahau hii nunua mojamoja kuna siksu unayatimbaa kavu
 
Edit:

9. Uchumi ukiruhusu tafuta chumba chenye choo ndani.

Kama uchumia na mazingira yanaruhusu, epuka nyumba zenye vyoo vya kushare. Kuna watu ustaarabu mdogo sana .

Kwa sasa nimeyatimba, ila kutaka kuforce kukaa Makongo Juu kumeniponza. Nikimaliza Kodi yangu naamsha.
Nunua kiwanja hata hatua 12 kwa 24.ujenge geto janja,acha utumwa,hizo laki sita utafyatua tofali kibao na kigeto ujanja kiko kama castle house full ujanja,hebu hizo posho unganisha ujenge geto ujanja au cheza mchezo wa kazini.
 
Dah muhimu sana.

Kuna nyumba nilikaa, choo cha kushare. Kuna mwamba alikua akiingia, ata kama kina maji yeye anashusha mzigo bila kumwaga maji.

Yaani ukiingia unaukuta mzigo pale, wakati maji sio kwamba hayapo.
Wengine hawajui mambo ya maji Waite uwape semina elekezi,jitahidi kujiongeza lakini pia geto janja waweza Jenga kwa pesa kiasi tuu
 
Mm mama mwenye nyumba ananiibia mabeki 3 zangu sio poa. Anawatafutia KAZI kwingine kisha uko anataka pesa ya nauli kwao ndio anawapeleka.mmoja kashindwa aliko pelekwa ndio kumpigia wife simu na kusema ilivyo kua. Na pia nackia mama mwenye nyumba kasema kua kila nikileta beki 3 atakua anawauza kwa wengine. Nimepata mzuka wa kumaliza kibanda changu ili mwezi ujao nisepe kwangu tu.
All the best
 
Kabla sijahamia hapa ninapoishi kwa sasa kuna sehemu nilikaa.

Wake wa wapangaji wenzangu wanakuja kupiga soga kibarazani kwangu.

Maji yalikatwa, wapangaji wakagoma kulipa hela yarudishwe.

Barabara kufika home changamoto kweli.

NIlipohamia kwa sasa mambo hayo hayapo. Shida ni mijusi ndio inanipa kero.
Sio mijusi hiyo broo. Kuna uzi humu si ukumbuki ila wanasema hizo ni antena/kamera za wenyewe.

Fanya jambo utashangaa wanahama wote.
 
Kuna watu hawataki kuacha alama ya kujenga nyumba hapa duniani. Nina rafiki mkaka, angeweza kujenga hata nyumba 3 ikiwemo ghorofa.
Ila hataki kusikia neno kujenga! Yeye anapanga nyumba nzuri za bei sehemu nzuri. Akichoka anakaa hotelini ndiyo maisha yake mwenyewe kayachagua.
Huyo jamaa yako mkumbushe kwamba ana miaka 50 mbele sasa asione hivyo alivyo ndivyo itakavyokuwa lawama hatutaki mwambie nimekwambia mimi lawama hatutaki na kama hataki mwache ainjoi ujinga.
 
Back
Top Bottom