Chrysanthemum
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 1,531
- 5,787
9: Usimle mpangaji mwenzio 🤣
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwahio hii Arsenal vs Man city huangalii?Sasa si atume screenshot. Jaman. Sema haujui balaa la umeme. Hapa umekatikd sijui umeisha me nimejikausha tu ndani.
Swali zuri mnoo.MImi sioni shida yake, ni lazima kila mtu ajenge nyumba? Biashara ya kupangisha itakufa. Duniani kote hii biashara ni kongwe, ana miradi yake mikubwa anajimudu kukaa popote. Unafikiri kuwa na nyumba ndiyo kuwa na maisha mazuri?
Ulivyo wa ajabu ukaondoka.Kuna nyumba nliishi ilikua nyumba ya familia ila kukawa na chumba kimoja ko mpangaji nipo mwenyewe, pale wakawa wananitreat kama Mtoto wa Ile familia palikua na mabinti wengi nkifua nguo zikikauka wanazitoa na kuzikunja jioni wananipatia palikua pazuri sema kipenge ikawa mambo ya ujana 'kuvusha' hawataki.
Sikuondoka, sema nkawa naleta mdada nastay nae siku mbili au tatu nakaaa wiki Moja au mbili naleta mwingine mpaka wakanizoea.....nlikaaa kama miaka miwili na miezi sitaUlivyo wa ajabu ukaondoka.
ungenivusha mie bichwa komwe niwe dem wakoKuna nyumba nliishi ilikua nyumba ya familia ila kukawa na chumba kimoja ko mpangaji nipo mwenyewe, pale wakawa wananitreat kama Mtoto wa Ile familia palikua na mabinti wengi nkifua nguo zikikauka wanazitoa na kuzikunja jioni wananipatia palikua pazuri sema kipengele ikawa mambo ya ujana 'kuvusha' hawataki.
Aisee! Sasa unakuwaje mpangaji wa masikini?Tatizo wenye nyumba wengi Dar ni maskini kuliko wapangaji.
Tujadili uwepo wa idadi kubwa ya wenye nyumba ambao ni maskini hapa Tanzania hasa jijini Dar
Nini kifanyike? Kiukweli idadi ya wenye nyumba maskini ni kubwa mno jijini Dar na miji mingine nchini kwetu. Je, ni mitazamo mibovu ya wananchi wengi kuhusu kumiliki nyumba? Yaani kwa haraka haraka kuna wapangaji wengi wana maisha mazuri kuliko wapangishaji. Maeneo ya uswahilini ni kawaida...www.jamiiforums.com
Refa kaharibu mechi. Arsenal alikuwa vizuri sana.Hii nipo Live Score naogopa kuangalia hii mechi.
CCM nini....Nilikua kwenye nyumba ya kupanga, nzuri tu. Tatizo mwenye nyumba akapandisha bei kwa asilimia zaidi ya 25, bila taarifa mapema.
Nikaona sio shida, nikahama mkataba ulivyoisha. Sasa katika harakati za kutafuta nyumba, kuna vitu nimejifunza na vingine nimeshachelewa nimejikuta najuta tayari niko ndani.
Baadhi yake:
1. Usikae na mwenye nyumba.
Nilipokua zamani nilikua sikai na mwenye nyumba. Anakuja mara chache sana. Ila sahivi nimeyatimba.
Hafu mwenye nyumba ana shughuli kila siku, mazingira yapo ovyo wala sio masafi kwasababu yeye tu ana ndugu zaidi ya 8 na watoto, ukijumlisha mnashare uwanja, aisee.
2. Jitahidi msiwe mna-share bili/matumizi ya maji au umeme.
Iwe na wapangaji wenzako au mwenye nyumba, jitahidi sana ulipie bili mwenyewe.
Ikitokea umebanwa sana bdsi angalau muwe wawili mwisho. Sub-meater hazitasaidia kitu. Mtatoa kila mtu 20,000/= ya umeme kwa mwezi wewe unashinda kazini ukirudi unawasha feni tu, kuna sista duu anachemsha maharage kwa presha cooker.
Lazima mtagombana tu.
3. Hakikisha nyumba imekamilika ujenzi, asikudanganye lipia tu namalizia wiki ili kuweka madirisha sijui.
Unavyoenda kukagua eti nyumba haijakamilika choo au dirisha, akasema lipia namalizia mtego huo.
Ukishalipia tu imeisha. Utakuta jikoni hakuna sink, feni ya sebuleni haweki, na ata maji unaweza kuta akachelewa kuyaingiza.
Jitahidi uende nyumba iliokamilika kila kitu.
4. Kama una gari, angalia upatikanaji wa funguo za geti.
Otherwise utajikuta unawahi kurudi kuogopa kufungiwa geti kama mtoto. Zamani nilikua ata saa 8 usiku naweza kutoka sahivi nawahi home saa 4 wasije funga geti. Nishalalamika ila ndio ivo, kila siku ahadi hewa.
5. Zingatia idadi ya wapangaji wenzako.
Kama unaweza, jitahidi wapangaji muwe wachache. Mkiwa kikosi kuna faida na challenge zake. Faida moja wapo unaweza pata mke hapo hapo. Ila hasara unakuta challenge hadi kwenye kamba za kuanika mfano weekend mkifua wengi kwa pamoja, makelele kila mtu akiweka singeli nk.
6. Uliza kuhusu utaratibu wa bili za maji taka, takataka/usafi na ulinzi shirikishi.
Hii michango haiwagi mikubwa ila nayo ni kero.
Kuna hii ya maji taka kuyatoa kwasababu shimo limejaa, michango ya wale wazoa takataka na ulinxi shirikishi.
7. Zingatia msimu wa mvua kunapitika? Mafuriko na nyumba kuvuja?
Kuna nyumba msimu wa mvua hazifikiki sio kwa gari wala kutembea, pia kuna uwezekano mvua ikinyesha nyumba ikawa inavuja.
8. Kelele/mishemishe za majirani.
Unaweza ukawa umeenda kucheki nyumba ukakuta pako cool, kumbe jioni kuna bar uchwara inapiga music usiku kucha.
Au ukakuta weekend au jioni ni nyumba za ibada wanatumia maspika ww unasema unapumzika wao wakakiwasha.
Edit:
9. Uchumi ukiruhusu tafuta chumba chenye choo ndani.
Kama uchumia na mazingira yanaruhusu, epuka nyumba zenye vyoo vya kushare. Kuna watu ustaarabu mdogo sana .
Kwa sasa nimeyatimba, ila kutaka kuforce kukaa Makongo Juu kumeniponza. Nikimaliza Kodi yangu naamsha.
Mijusi ni changamoto ht hapa nilipo ni wengi....puliza runguKabla sijahamia hapa ninapoishi kwa sasa kuna sehemu nilikaa.
Wake wa wapangaji wenzangu wanakuja kupiga soga kibarazani kwangu.
Maji yalikatwa, wapangaji wakagoma kulipa hela yarudishwe.
Barabara kufika home changamoto kweli.
NIlipohamia kwa sasa mambo hayo hayapo. Shida ni mijusi ndio inanipa kero.
Ili ukichelewesha kodi asikusumbue?Cha kuongezea usipange nyumba ambayo mwenyenyumba Hana kazi yani anategemea hela ya kodi