Kama unataka kulala njaa tegemea pesa ambayo ipo kwenye mfuko wa mwenzako

Kama unataka kulala njaa tegemea pesa ambayo ipo kwenye mfuko wa mwenzako

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Kama unataka kulala njaa tegemea pesa ambayo ipo kwenye mfuko wa mtu mwingine.

Usiache jua lizame kwa kuendelea kusubiri hela ambayo umeahidiwa kupitia kauli zifuatazo;

(a) "Usijali leo uhakika nitakutumia baadae"😃
(b) "Nipo somewhere hakuna huduma ya pesa, nikirudi nitakutumia"😃
(c) "Nitumie namba yako ili baadae nikutumie".😃
(d) "Kuna mishe naisikilizia ikitiki nakutumia fasta".😃
(e) "Nipo kwenye kikao/msibani/darasani/mpirani/kanisani/, nikitoka nitakutumia".😃


Pesa yako ni ile ambayo ipo kwenye mfuko wako. Lakini pesa ambayo ipo kwenye mfuko wa mwenzako hata kama ulimwambia akushikie au ulimkopesha, hiyo si pesa yako na ukiitegemea ikulishe hakika utalala njaa.

RIGHT MARKER
Dar es salaam
 
Kinachokera zaidi iwe ni hela yako halali uliyomkopesha muhusika 🐼
 
Watu wengi wenye kuahidi ni watu wenye moya safi tu isipo kuwa wanapitia hari ambazo hawawezi kusema hapana kwan kimtizamo wameshawaaminisha mambo safi.
Ni kweli mm huwa nakuwa guilty pale ninaposhindwa kumsaidia anayehitaji

Ninapomsaidia mtu napata amani Sana
 
Kinachokera zaidi iwe ni hela yako halali uliyomkopesha muhusika 🐼
Hela uliyompatia mtu haijalishi unaimiliki kwa hisia gani ili mradi haipo kwako sio yako muda huo
 
Back
Top Bottom