Kama unataka kuwa na Fikra Tulivu fanya mambo haya mawili

Kama unataka kuwa na Fikra Tulivu fanya mambo haya mawili

Joined
Nov 24, 2024
Posts
26
Reaction score
35
1)Elewa ukomo wa fikra,

Ni mambo mengi yanajiri katika maisha yetu, Si yote tunauwezo wa kuyadhibiti tupendavyo katika uhalisia.

Lakini fikra zetu zimebeba vita kubwa ambazo mikono yetu haiwezi pigana.

Hali hii imejaza ukungu katika mawazo yetu ambapo hutufanya tuteseke kimawazo na kihisia sababu tunapambana na mambo yaliyo nje ya uwezo wetu.

Namna pekeeya kupunguza makali hayo ni kuweza kutofautisha uwezo wako thabiti katika kuishi na upi ni mtiririko wa mawazo na hisia.

2)JENGA UBORA WA FIKRA UZITAKAZO.

Kama ilivyo miili yetu binadamu tusipo itunza Kwa kuilisha vizuri, kufanya mazoezi nakadhalika matokeo huwa si mazuri magonjwa harufu mbaya nakadhalika.

Hivyo hivyo hata katika fikra zetu tusipo zitengenezea mazingira mazuri hatuwezi epuka athari hasi zitakazo tokana na matendo yetu.


Swali kwako: Ni jambo gani Lina kusaidia kukaa sawa Mentally.
 
Bangi mkuu yani hakuna mtu anaeweza kwenda deep kwenye meditation kama mvutaji wa bangi....

NB:Nimesema mvutaji wa bangi sio muathirika wa bangi...
 
Back
Top Bottom