Kama ungependa kuacha legacy imara zaidi wekeza kwenye umiliki wa digital assets pia

Kama ungependa kuacha legacy imara zaidi wekeza kwenye umiliki wa digital assets pia

miamiatz

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
505
Reaction score
941
Kuna baadhi yetu tunaowaza kujenga kwa ajili ya familia. Kununua viwanja kwa ajili ya familia. Kunununua mashamba kwa ajili ya familia. Ni jambo jema sana ila tunasahau kuwekeza kwenye digital assets kwa ajili ya familia.

Digital assets ni assets zote za kiteknolojia ambazo asilimia kubwa sio physical. Mfano JF ni digital asset ya waanzilishi wake Mkuu Melo na Mushi. Video na audio mbalimbali zilizopo youtube na kadhalika ni digital assets za wamiliki wake.

Blogs mbalimbali ni digital assets za wamiliki wake. Hata fb ni digital asset ya Zukckerberg. Google ni digital asset ya Page na Brin. Softwares mbalimbali ni digital assets. Apps mbalimbali ni digital assets.

Kwasasa bado Tanzania tupo nyuma kwenye nyanja ya digital. Ila baada ya miaka kumi mbele wengi tutajilaumu kwanini hatukuwekeza kwenye hii sekta.

Katika uzao wako wapo watakaonufaika sana na uwepo wa physical assets na wengine digital assets. Wewe kama wewe unaweza kosa njia ya ku monetize kwa kiwango cha juu ila kwenye uzao wako akatokea atakaeona njia bora zaidi ya ku monetize hiyo digital asset.

Kwa mfano kuna watu wanaangalia domains zote nzuri nzuri wanazisajili na kuzimiliki ila hawaweki content.

Baada ya miaka kadhaa unakuta kuna kampuni inahitaji kuinunua hiyo domain basi unakuta inauzwa kwa millions za kimarekani. Ukigoogle most expensive domains utapata picha ya kile nimemaanisha hapa.

Please share maoni yako katika mada hii. Sijakusudia maoni yangu yawe kamili bali nimekusudia kuanzisha thread wengine wajazie. Asante.

Courtesy of miamiatz
 
Ahsante mkuu kwa hili wazo. Wengi tumeaminishwa kuwekeza kwenye "tangible assets" hasa real estate. Hilo ni jambo zuri, ila tunapaswa kufikiri hatua mbili mbele kwa kuwekeza kwenye digital assets kwa kuwa matumizi ya teknolojia yanazidi kushika kasi kila siku.
 
Ahsante mkuu kwa ufumbuzi mzuri coz kwa sasa kwa wengi nikama tuko usingizini ila miaka 10 ijayo,mambo yanakuwa mengine coz e-commerce imeshika kasi sana
 
Back
Top Bottom