Kama ushapitia hatua hata moja kati ya hizi wewe ni chizi

Kama ushapitia hatua hata moja kati ya hizi wewe ni chizi

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2014
Posts
4,298
Reaction score
7,612
Inasemekana kila binadamu ana ka uchizi ndani yake level ndo hutofautiana na chizi sio mpaka aokote makopo!

1. Kama umewahi kushika kopo la maji bafuni na kuhesabu 1, 2 mpaka 3 ndo ukajimwagia huku ukiruka ruka wewe ni Chizi.

2. Kama umewahi kutumia line yako no 1 kujipigia kwenye line yako no 2 wewe ni chizi.

3. Kama umewahi kuongea peke yako ghafla ukaona mtu anakuangalia ukazuga unaimba wewe ni chizi.

4. Kama uliwahi sahau pesa yako kwenye mfuko wa nguo ukaja kuiona wakati wa kufua ukafurahi sana na kuhisi kama mtu kakuhonga wewe ni chizi.

5. Kama uwa unaongea na mende au panya tena unamuuliza maswali kabla hujamuua wewe ni chizi

6. Kama umewahi Ku balance switch ya taa katikati ili uone kama taa itazimika au itaendelea kuwaka wewe ni chizi
 
Back
Top Bottom