Kama Uwanja wa Benjamin Mkapa una jumla ya Taa 248 kwanini zinazowaka ni 124 tu?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Yaani Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bwana Said Yakubu ni kweli hujui kwanini Taa hizo Nusu ndiyo huwashwa kama ulivyotanabaisha katika Mkutano wako na Waandishi wa Habari leo?

Sasa Mimi GENTAMYCINE kabla sijakupa Jibu kwanini Taa ziko 248 kwa Ujumla wake pale Benjamin Mkapa Stadium na zinazowaka na kutumika ni Nusu yake ( yaani 124 ) tu nakuomba Kwanza Kesho au Siku yoyote Kaangalie kama hata hizo Taa 124 zisizowashwa zipo.

Cheza na Wote, ila siyo Watanzania!!!
 
Inasemekana taa zinanguvu sanaa yaani tukikadiria mechi za usiku ukitoa dk 90 ukiongeza na dk za maandalizi ya uwanja mpaka mechi inaisha tufanye masaa 5 inaweza kugharimu hata zaidi ya milioni 20 Kwa gharama ya unit za umeme kwa taa zote hizo

Ndio maana wanaziwasha nusu nusu Kwa kukadiria gharama isiwe kubwa,

All in all uwanja unatakiwa marekebisho, mageti yaongezwe na vitu vingine Kama hivyo taa za uwanja na miundo mbinu yote ya uwanja

Uwanja unaonekana mkubwa tu lakini hauna akili
 
Acha uongo!
 
Ukisikia inasemekana basi kaa kitalaamu....

Hafu hii sio tunapangwa yahn taa zuwake 124 out 248 exactly nusu hii.
 
Bilioni 31 ni wizi. Mama yupoyupo tu watu wananyoosha.
 
Usionyeshe ujinga wako hadharani kaa nao ndani.
Yani shilingi bilioni 31 za Tanzania ukarabati una ona nyingi wakati ujenzi mwaka 2004 ulikuwa dollar za Marekani milioni 60 sawa na shilingi bilioni 129 za Tanzania wakati huo.
Ambazo kwa sasa ni sawa na shilingi bilioni 248 za Tanzania, hivyo ukarabati wa uwanja kwa ajili shilingi bilioni 31 ni hela ya kawaida mno kwa sasa.
Kwa akili yako ndogo elfu kumi ya mwaka 2004 ni sawa na elfu kumi ya mwaka 2023 katika manunuzi ?
Bei ya vifaa vya ujenzi mwaka 2004 ni sawa na mwaka 2023 ,?
Mwaka 2004 dollar moja ya Marekani ilikuwa ni shilingi 1200 leo mwaka 2023 dollar moja ni sawa na 2440.
Sasa chukua dollar milioni 60 za mwaka 2004 ambazo zilijenga uwanja zidisha mara 2440 ndio bei halisi ya ujenzi wa Uwanja kwa mwaka 2023.
 
Uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…