Kama vile uwepo wa hospitali unaonyesha uwepo wa magonjwa, uwepo wa polisi ni ishara ya ukosefu wa amani na utulivu

Kama vile uwepo wa hospitali unaonyesha uwepo wa magonjwa, uwepo wa polisi ni ishara ya ukosefu wa amani na utulivu

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Kama vile uwepo wa hospitali unaonyesha uwepo wa magonjwa, uwepo wa polisi ni ishara ya ukosefu wa amani na utulivu, Wingi wa polisi katika nchi ni ishara ya amani ndogo zaidi, level za ukosefu wa amani zinatofautiana, Wenye amani hawahitaji polisi na mahakama. Amani tuliyonayo inayolindwa kwa mtutu wa bunduki si amani halisia ni ya muda na hutoweka. Amani ya kweli hutoka ndani , huzalishwa ndani ya moyo wa mtu inayomsukuma kutenda mambo mema na yenye adili.

Na maadili na amani hii inapomomonyoka hakuna mtutu wa bunduki unaoweza kuilinda. Mihimili itatingishwa na kuyumba na dunia itakuwa sehemu ya chaos. Kwa watu lazima wawe trained to be good kama tunataka amani ya kweli na tusitegemee polisi na mahakama, watu hao na uwepo wao unatokana na uovu. Na udhibiti wa uovu kwa kutumia bunduki ni wa muda tu. Msisitizo ni kujenga character za watu wetu kuwa bora na wenye tija.

Injili lazima ihubiriwe sio ya kupuuza. Narudia tena tabia za watu zinapoharibika na kuwa za uovu kwa wingi wao na kama watu hawatolelewa vizuri katika malezi bora hakuna polisi itakachoweza kufanya kulinda hiki kinachoitwa amani kwasababu na wao hawako immune to deterioration. They can deteriorate also.
 
Back
Top Bottom