Kama vitambulisho vya NIDA havifanyi kazi, tusitishe mchakato huo

Kama vitambulisho vya NIDA havifanyi kazi, tusitishe mchakato huo

OLS

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2019
Posts
426
Reaction score
685
Je, vitambulisho hivi kazi yake ni nini? Kwanini vinaonekana ni muhimu kwa wananchi na sio kwa serikali kiasi cha serikali kuleta uzembe wa utoaji wa vitambulisho hivi?

Nilidhani NIDA ingewezesha mambo haya
Kwanza niseme nilipongeza mchakato huu na nilikuwa wa kwanza kupanga foleni kipindi kile usiku ili kuweka taarifa zangu kuwekwa kwenye database, ilikuwa mwaka 2011 kama sio 2012, lakini nililazimika kuweka taarifa upya 2015. Sio shida nilidhani haya

1. NIDA kupunguza uhitaji wa utitiri wa vitambulisho
Hapa nilijua wingi wa taarifa zinazochukuliwa na NIDA zinatosha kuondoa adha ya vitambulisho vya serikali kama vya mpga kura na nk. Nilikuwa kati ya watu wa kwanza kuhoji utofauti wa kitambulisho cha mpiga kura na NIDA kiutendaji, swali ambalo halijajibiwa hadi leo.

2. Kutambua wahalifu.
Kwa kuwa NIDA wanachukua fingerprints, nilijua ni rahisi watu wakifika eneo la tukio kukusanya fingerprints na kuscan kujua aliyefanya tukio hilo, kama ilivyo kwa walioendelea. Hata hivyo suala hili limekuwa kizungumkuti, kwa kuwa sasa mtu anaweza kaa hospitali miaka na wenyewe wanasema nduguze hawajamtambua, maana yake hata serikali imeshindwa kumtambua mtu huyo mbali na kuwa ana vidole vyake hapo alipo ni suala la kuscan ili kumtambua ni nani na alipotokea.

USHAURI WANGU
NIDA inaweza kutatua matatizo mengi sana. Lakini kwa sasa serikali ni kama haioni umuhimu wa vitambulisho na hivyo kumekuwa na uzembeaji mwingi sana kwenye utoaji wa vitambulisho. Nashauri haya...

Kila mtanzania apewe kitambulisho hicho ndani ya wakati na kiweze kuwa upgraded inapotokea kimechakaa. NB: Ni kila mtanzania sio mwenye miaka 18 kwenda mbele kwa kuwa hata mwenye umri chini ya miaka 18 ni mtanzania. Kiumbe ambaye tunaweza kusema hatujui uraia wake ni aliyetumboni tu. Hivyo wote wanastahili kupata kitambulisho.

Vitambulisho vikusanye taarifa nyingi iwezekanavyo na kusiwe na mbambamba, NIDA iwe ni taasisi pekee yenye taarifa za watu na taasisi nyingine ambazo mtanzania ataridhia zitachukuliwa kutoka NIDA bila kuwa na mlolongo mrefu wa barua ya mtendaji, muhuri wa nani, kiapo cha mzazi, cheti sijui cha nini nk.

Let the technology work for us.

Signed OLS
 
Nakubaliana na wewe mtoa mada. Katika suala hili la vitambulisho kutoka NIDA, kuna uzembe wa hali ya juu. Tangu 2017 Novemba niliposajili hadi leo sijapata kitambulisho cha taifa!!!! Na hakuna sababu za msingi kwa nini vinachelewa hivyo. Nimekuwa nikifuatilia kwa nyakati tofauti ofisi za NIDA, kila nikienda naambiwa bado kitambulisho hakijatoka.
 
Nakubaliana na wewe mtoa mada. Katika suala hili la vitambulisho kutoka NIDA, kun uzembe wa hali ya juu. Tangu 2017 Novemba nikiposajili hadi leo sijapata kitambulisho cha taifa!!!! Na hakuna sababu za msingi kwa nini vinachelewa hivyo
Wewe itakua Mrundi wamekustukia [emoji1787] rudi kwenu Bujumbura
 
Back
Top Bottom