Kama Wachezaji wa Simba wataendelea kucheza 'Show Game', kwenye Makundi nje na kwenye ligi hawapati kitu

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
4,445
Reaction score
4,707
Nimekata tamaa ni wachezaji wa klabu ya Simba kutoka na aina ya uchezaji wao wa kutaka kushangiliwa "Show game".

Wachezaji hawajui kuwa kila dakika timu inataka goli wanatumia muda mwingi kupiga chenga zisizo na tija kwa timu.Wachezaji hawapigi mashuti wanapiga chenga na kupoteza mipira.

Kwa walioona mechi ya leo kati ya Simba na Bandari , Wachezaji wa Bandari walikuwa nyuma lakini wamecheza kwa malengo na kusawazisha goli na kuongeza bao la ushindi.

Naamini ingekuwa Bandari ndio imeanza kufunga kwa wachezaji wa Simba wasingeweza kusawazisha lile goli kwa wanapenda kucheza "Show game".Hitimisho kwa uchezaji huu Simba itatolewa Mechi za Makundi na Ligi kuu ya Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ni mfumo wa mwalimu, Simba ya Leshante na Masoud haikuwa inacheza show game.

Labda niseme hivi kama mashindano ya level hii yanatushinda kuna maajabu gani tuyakayoyafanya kwenye klabu bingwa Africa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rambirambi ya mafisango imeanza tena

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inaitwa tiki taka, ni style inayopendwa na Barcelona ila inataka wachezaji wenye uelewa mkubwa wa mchezo na wanaoelewana wenyewe kwa wenyewe kwa kiasi kikubwa.

 
Wachezaj wa simba hawana umakini simba hawana wachezaj wa kuamua matokeo coach nae hana mbinu mbadala
 
Wachezaj wa simba hawana umakini simba hawana wachezaj wa kuamua matokeo coach nae hana mbinu mbadala
Kwangu mimi sina tatizo na wachezaji, nna tatizo na kocha, uwezo wake ni mdogo sana.

Wachezaji wanafuata mbinu za kocha kama kocha anashindwa hata kufanya sub za maana tangu ameingia Simba utamlaumu nani.

Mpaka sasa Simba imeshiriki makombe kadhaa chini ya huyu kocha na inaishia njiani. Msiniambie tunajiandaa na klabu bingwa ya Africa that's nonsense.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
😁😁😁 kila mtu atavuna anachopanda
 
Kuhusu coach n Kweli tunahitaj coach kwa ajili ya kubeba mataj nasio coach wa kuchezea Mpira show game Pia tunahitaj wachezaj makini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…