Wanabodi,
Najua wengi wetu wameumizwa sana na kifo cha kikatili cha Mzee Ali Mohamed Kibao, natoa tena pole kwa wote.
Watu wamekasirika hadi kuwasomea Albadir, hivyo naomba kuwaelimisha kidogo kuhusu wauaji na utendaji kazi wa Albadir ambayo inafuata kanuni ya karma.
Kama wauawaji hao ni watu "Wasiojulikana", then karma na Albadir itawahusu, na watalipwa kwa matendo yao na uovu wao, lakini kama waliofanya mauaji hayo ni watu 'wasiojulikana', then sio karma wala Albadir inaweza kuwafanya chocolate, kwasababu walikuwa wanatimiza wajibu wao!.
Naomba kujitambulisha tena na tena ili kusaidia kuwaelimisha wengine kuhusu utendaji kazi wa kitu kinachoitwa "the operatives", mimi nimezaliwa na wazazi wangu wote wawili, Baba na mama ni waserekali.
Serikali zote duniani zina utaratibu wake wa kufanya kitu kinachoitwa "elimination" of dissidents. Ile mwaka 1976 kwenye ile kesi ya mauaji Mwanza, Mzee wangu alihusika na mimi kuzishuhudia baadhi ya zana za kazi baba akirudi nazo usiku mkubwa. Nawaomba mkisikia baadhi ya maofisa wa jeshi, polisi na usalama wa Taifa wanakuwa walevi wa kutupa, wasameheni, Mambo wanayoyapitia ili kujisahaulisha lazima wawe bwii!.
Hivyo kuna watu wanaajiriwa na kupewa mafunzo rasmi ya elimination. Majeshi yote yana watu hawa, wanaitwa wadunguaji, snipers, hivyo hata mimi nikiwa jeshini JKT Makutopora kwa mujibu wa sheria, kwenye somo la range, nilihit the bull 9/10, hivyo nilipomaliza tuu jkt nilipelekwa moja kwa moja JWTZ, Airwing na huko tukaanza moja deployed nyingine ya jeshi. Huko sasa nikadungua 10/10, Mmoja wa waalimu wangu Afande Kahamba, Sstg. akatufubdisha kuwa kazi ya polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zake, kazi ya usalama wa Taifa ni kulinda Serikali iliyopo madarakani na kazi ya jeshi ni kulinda nchi. Kwa upande wa jeshi shughuli kuu ya askari jeshi ni kuua tuu, nothing more nothing less!. Nikaanza kulichukia jeshi!.
Kumbe kambi hiyo ya Airwing ndipo wanapoendeshea Mahakama ya Kijeshi Court Marshall nikashuhudia kalinye kalinye za maofisa wa jeshi wakihukumiwa Mahakama ya Kijeshi, kiukweli niliaga jeshi kwa amani nikaenda kujiunga na TSJ nikawa mwandishi wa habari na mtangazaji.
Sasa kwenye hizi eliminaons ziko mbinu mbalimbali za eliminaons naomba hapa nisizitaje ila hakuna justification yoyote kumuua binadamu kwa ukatili wa kiasi kile.
Sasa kwa vile kuna watu jukumu lao ni kuua, watu hao wakitumwa kumuua yoyote, sio jukumu lao kujua amefanya nini, wao wakipewa amri halali ya eliminaons, kazi yao ni tu eliminate, how, ni juu yao!.
Hivyo kwenye Utekelezaji wa eliminaons wao wanatimiza wajibu wao, hivyo kama mlengwa was shortlisted kwenye list ya eliminaons, na akawa eliminated, karma ya eliminaons haiwahusu, hata msome Albadir haiwahusu kwasababu wao walikuwa wanatimiza tuu wajibu wao!.
Ndio maana nimesema kama waliofanya ukatili huu ni watu "wasiojulikana" then karma na Albadir itawahusu lakini kama ni 'wasiojulikana', karma wala Albadir haiwahusu!.
Ila ili eliminaons ifanyike kihalali, lazima CinC asaini death warrant ya hiyo operation ya eliminaons.
Askari polisi, jeshi na usalama wa taifa, wanapoau kwenye kutimiza majukumu yao, sio dhambi!, hata vifo vya watu wasio na hatia, vinapotokea kwenye operations zozote, hatia ya damu isiyo na hatia sio kwa watekelezaji bali kwa waliopanga na kutoa amri ya Utekelezaji!
Kwa wasio jua tofauti kati ya "wasiojulikana" na 'wasiojulikana' karibu pande hii
Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana
Wasalaam
Jumatano Njema.
Paskali