Kama wamegoma kusajili Umoja Party tuhamie TLP

Kama wamegoma kusajili Umoja Party tuhamie TLP

Johnny Sack

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2017
Posts
8,984
Reaction score
19,288
Chama cha Umoja Party ambacho ndio kilikuwa chama cha kutetea legecy ya Jemedari Hayati Magufuli kimekataliwa kupewa usajili licha ya kuwa na vigezo vyote

Ni dhahiri serikali ya sasa inaogopa nguvu ambayo chama hiki kingekuwa nayo na kingeitoa CCM madarakani

Sasa kwa kuwa chama cha TLP kilikuwa chama rafiki wa JPM na hata kipindi kile kukiwa na tishio kuwa CCM isingempa JPM muhula wa pili, Mwenyekiti wa TLP Augustino Lyatonga Mrema (RIP) alitamka wazi wazi bila kuogopa kuwa kama CCM wasingempa JPM nafasi basi TLP ingempa
Hii inaonyesha ni jinsi gani TLP unavyoendana na falsafa za JPM

Natumaini Polepole, Bashiru, Luhaga Mpina, Ndugai, Msukuma na wanamapinduzi wengine tutajiunga na hiki chama kuendeleza legacy ya JPM
20220419_125518.jpg
 
Tukihamia hiyo sijui tlp ya Mbatia yatahamia huko pia, kwa kifupi ukiona Serikali inatumia nguvu ujue haikubaliki na Wananchi, kilichopo ni lazima tu, lkn swali ni kwamba hiyo lazima mpaka lini? Wamefikia mahali mpaka Spika wa Bunge anatishia watu, Power yao imekaribia mwisho kwani hata kwa Mzungu nako nafikiri mambo siyo tena, it’s over!
 
Vyama vilivyopo vinatosha cha msingi mvipe nguvu Ili waisimamie serikali VIZURI!!

Wazo lako ni zuri lakini mngepigania Katiba kwanza Ili tupate viongozi Bora pia fedha zetu za ule mchakato wa Katiba Mpya zisiende Bure!!
Sasa tutapigania Katiba mpya bila kuws na platform?
 
Chama cha Umoja Party ambacho ndio kilikuwa chama cha kutetea legecy ya Jemedari JPM kimekataliwa kupewa usajili licha ya kuwa na vigezo vyote

Ni dhahiri serikali ya sasa inaogopa nguvu ambayo chama hiki kingekuwa nayo na kingeitoa CCM madarakani

Sasa kwa kuwa chama cha TLP kilikuwa chama rafiki wa JPM na hata kipindi kile kukiwa na tishio kuwa CCM isingempa JPM muhula wa pili, Mwenyekiti wa TLP Augustino Lyatonga Mrema (RIP) alitamka wazi wazi bila kuogopa kuwa kama CCM wasingempa JPM nafasi basi TLP ingempa
Hii inaonyesha ni jinsi gani TLP unavyoendana na falsafa za JPM

Natumaini Polepole, Bashiru, Luhaga Mpina, Ndugai, Msukuma na wanamapinduzi wengine tutajiunga na hiki chama kuendeleza legacy ya JPMView attachment 2377627
Nchi ina wapumbavu wengi sana, wengine ni nyinyi mnaojiita Umoja Party ambao mnamuabudu magufuli
 
Magufuli anayo "legacy". Je yatosha kuwa ndio msingi mkuu wa kuanzisha chama?
 
Back
Top Bottom