Makambovich
JF-Expert Member
- Oct 27, 2018
- 207
- 200
Tumeangalia mechi ya Al Alhy na Simba huku wachezaji wazawa watatu tu Aishi Manula, Jonas Mkude na Rashid Juma wakipata nafasi ya kuanza wengine waliobaki ni hawa tunaowaita wa kimataifa, kwa muda mrefu tuliamini tunafungwa na timu za wenzetu sababu ya kukosa wachezaji wa kimataifa wakusaidia vilabu vyetu kwenye mechi za kimataifa, ukiangalia mechi mbili za ugenini walizocheza Simba ni wazi kuna haja ya benchi la ufundi likapitisha panga kwa baadhi ya wachezaji wa kigeni na kubaki nao wachache watakao leta ufanisi.
Najua kwa wale madalali wa 10% za wachezaji sio jambo jema kwao ila kwa manufaa ya timu ni heri kuwa na wachezaji 5 wenye uwezo mkubwa kuliko kundi kubwa la watalii.
Kwa mtazamo wangu wadau turudishe ile kanuni ya mapro watano