Kama wanashindwa kutusaidia kwenye mechi za kimataifa kuna haja gani ya kuwa na Mapro wengi kwenye vilabu vyetu

Makambovich

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2018
Posts
207
Reaction score
200
Tumeangalia mechi ya Al Alhy na Simba huku wachezaji wazawa watatu tu Aishi Manula, Jonas Mkude na Rashid Juma wakipata nafasi ya kuanza wengine waliobaki ni hawa tunaowaita wa kimataifa, kwa muda mrefu tuliamini tunafungwa na timu za wenzetu sababu ya kukosa wachezaji wa kimataifa wakusaidia vilabu vyetu kwenye mechi za kimataifa, ukiangalia mechi mbili za ugenini walizocheza Simba ni wazi kuna haja ya benchi la ufundi likapitisha panga kwa baadhi ya wachezaji wa kigeni na kubaki nao wachache watakao leta ufanisi.

Najua kwa wale madalali wa 10% za wachezaji sio jambo jema kwao ila kwa manufaa ya timu ni heri kuwa na wachezaji 5 wenye uwezo mkubwa kuliko kundi kubwa la watalii.

Kwa mtazamo wangu wadau turudishe ile kanuni ya mapro watano
 
Mmisri aliyeambulia droo Tanzania Ni Almasri tu. Halafu hao mnaowataka wa level za juu mmoja auzwa bilioni kwenda juu. Msitake kuweka vigezo vikuuubwa kumbe heka kiduchu
 
Panga lipite kwa gyan,kotei,kwasi,zana,niyonzima sioni umuhimu wa kuwafuga hawa watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabisa kwa mechi mbili za ugenini tumeona wazi hatuna mapro hawa wanatudanganya tunapocheza na Singida Utd au KMC lakini wanapokutana na wenzao wanaojua hakuna kitu
 
Tumeangalia mechi ya Al Alhy na Simba huku wachezaji wazawa watatu tu Aishi Manula, Jonas Mkude na Rashid Juma wakipata nafasi ya kuanza wengine waliobaki ni hawa tunaowaita wa kimataifa, kwa muda mrefu tuliamini tunafungwa na timu za wenzetu sababu ya kukosa wachezaji wa kimataifa wakusaidia vilabu vyetu kwenye mechi za kimataifa, ukiangalia mechi mbili za ugenini walizocheza Simba ni wazi kuna haja ya benchi la ufundi likapitisha panga kwa baadhi ya wachezaji wa kigeni na kubaki nao wachache watakao leta ufanisi.

Najua kwa wale madalali wa 10% za wachezaji sio jambo jema kwao ila kwa manufaa ya timu ni heri kuwa na wachezaji 5 wenye uwezo mkubwa kuliko kundi kubwa la watalii.

Kwa mtazamo wangu wadau turudishe ile kanuni ya mapro watano
Wawe watano lakini wacheze watatu hasa kwenye ligi yetu. Huko nje ya nchi kuna utaratibu mwingine
 
Simba ilifika hatua ya nusu fainali Klabu bingwa Afrika 1974 ikiwa na wazawa watupu pamoja na kocha mzawa Paul West Gwivaha.
Mwaka 1993 Simba ilifika hatua ya fainali kombe la CAF ikiwa na kikosi kikali kabisa kilichoundwa na wazawa wutupu chini ya kocha mzawa Abdallah King Kibadeni.
Labda nyakati zimebadirika, lakini ikiwa ni hivyo, wachezaji wa kigeni waliopo Simba na ambao wana ni sifa wawili tu. Okwi na Chama waliobaki ni wa kawaida sana

Sahihi kabisa ni ngumu kwa mchezaji mzawa kufanya vyema kwa msimu zaidi ya miwili mfululizo, wengi wanapotea mwisho wa siku tunaletewa hawa mapro ambao hawapo hata kwenye timu zao za Taifa
 
Back
Top Bottom