GE2025 Kama watoto wanakusanywa kwenye kampeni, basi waruhusiwe kupiga kura

GE2025 Kama watoto wanakusanywa kwenye kampeni, basi waruhusiwe kupiga kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Haya sio mawazo yangu, ni mawazo ya mdau mmoja ambaye ni mwanaharakati wa watoto, ameshangazwa na baadhi ya vyama kukusanya watoto kwenye mikutano ya kampeni zao.

Watoto hawa hukusanywa kama mafungu ili kuweka wingi kusikiliza ahadi za wagombea lakini hawana uwezo wa kuuliza maswali wala kupiga kura. Hata hivyo watoto ni muhimu kwenye kuongeza wingi.

Kwa mujibu wa mdau ni kuwa, watoto kukusanywa mikutanoni ni suala la kuwadharirisha kwa kuwanyima haki yao ya kucheza na kukua. Hivyo amesema kama wanakusanywa kwenye kampeni basi pia waruhusiwe kupiga kura maana ni suala la ajabu kujaza watoto kwenye kampeni huku ukitaka watu wazima ndio wapige kura.

Kwa niaba ya mdau
 
Back
Top Bottom