Kama watu hawaandikishwi wakiingia lock-up basi ni ngumu kutrace kuhusu akina Ben Saanane, Azory, n.k

Kama watu hawaandikishwi wakiingia lock-up basi ni ngumu kutrace kuhusu akina Ben Saanane, Azory, n.k

NewPage

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2021
Posts
1,321
Reaction score
2,106
Yaani Wanasheria wa Serikali walinishangaza sana kuleta ushahidi ambao unaonesha watu hawakuwekwa lock-up pale TAZARA wakati wahusika wanajua kabisa waliwekwa lock-up hiyo.

Mashahidi wa Serikali walishadadia sana kwa ushahidi wa sijui Jumanne yule kuonesha kuwa eti watuhumiwa hawakuwa lock-up ya TAZARA.

Yaani hata nafsi na mioyoni mwao wanajua ukweli huu dhahiri kabisa kuwa waliwaweka hawa watuhumiwa lock-up ya TAZARA bila kufuata taratibu za kuwaandikisha ili isijulikane kabisa wako wapi.

Walifikia mpaka kuamua kuwapa watumiwa majina ya bandia ili hata kule Mbweni wasijulikane kama wapo! Hii yote ilimradi tu kuwaficha.

Tena kama inawezekana zile dentition register za Mbweni zingepatikana ingejulikana kabisa kuwa watuhumiwa waliandikishwa kwa majina bandia.

Serikali mnataka nini na kesi hii mbaya inayozidisha chuki hapa nchini mwetu. Tayari ubaya wa akina Kingai na kundi lake unajulikana.

Utaratibu wa utendaji wao hauwezi kamwe kuwakwepesha na kupotea kwa akina Ben Saa 8 na Azory! Ni suala la muda tu - kila kitu kitakuja kuwa wazi na Rais wangu Samia nina uhakina anawacheki tu mnavyombwela mbwela!
 
CCM inaendeleza utawala wa ki fashist uliyopelekea mabadiliko makubwa Ulaya wananchi walipambana kudai demokrasia.

Kuongezea wananchi kodi pasi na kuboresha maisha yao. Wapinzani wanaishi kama 2nd class citizens, wanapewa baadhi ya haki lakini wana CCM wanapewa haki zote.
 
Tanzania tuna polisi wahuni sana, yani ndio maana hakuna askari polisi anayeheshimika huku mitaani na wakistaafu ndio kabisa huwa wanapotea . Polisi watu wabaya sana.
Hakika!
 
CCM inaendelea a utawala wa ki fashist uliyopelekea mabadiliko makubwa Ulaya wananchi walipambana kudai demokrasia.

Kuongezea wananchi kodi pasi na kuboresha maisha yao. Wapinzani wanaishi kama 2ns class citizens, wanapewa baadhi ya haki lakini wana CCM wanapewa haki zote.
Yaani - hivi unajua bei ya petrol kuanzia jana au bado unatumia uliyojaza mwezi jana?
 
Back
Top Bottom