Kama Wewe Ni Mhenga Pita Hapa Uchukue Zawadi Yako

Castr

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
35,012
Reaction score
70,201
Heshima kwenu wadau.

Nimekuja kukuonyesha na kukupa miongoni mwa nyimbo zilizotamba miaka hiyo. Miongoni kuna hadi nyimbo za kwanza za baadhi ya wasanii.

Wengine hawatakuja kutoa wimbo mkali kama ambao nitaweka hapa.

Enzi hizo za kusikiliza Radio kuna nyimbo zilikua zinachezwa halafu unapata picha hawa jamaa ni washua. Hapa kuna Big Jah Man

Halafu na Dolphin Pose

Mwingine ni Dataz.

Wanamuziki wengine hawatokuja kutoa ngoma nzuri tena hata wafanyaje kuna Fid Q na Fid q.com, K Basil na Ridhiki halafu Mh Temba na Wimbo wa Nakumaindi.

Halafu kuna zile ngoma kali ambazo zinakutikisa kichwa bila kutaka.
Kuna kamanda ya Daz Nundaz, Mr 2 Niamini na Crazy GK na Tutakukumbuka.

Kuna wasanii walitamba lakini walikua na genre yao kabisa kabisa, mfano Kali P na Dudubaya.

Kwa wanaojua hip-hop kwa Tz watajua waanzilishi ni HBC na Prof Jay.

Kuna kipindi kikaja cha kuusiana kuhusu ulevi, Suma G akaimba Pombe, Solid Ground wakatoa Athman Mlevi, halafu wakausia kuhusu michepuko na wimbo Baba Jeni.

Kuna mshkaji alifanya kama mapinduzi hivi akatoa wimbo unaitwa Baby Gal, yeye anaitwa Mad Ice.

Kuna ving'ang'anizi wa kwenye fani. Mmojawapo Dully Sykes na Madii.

Airtel wanasena nimetumia 90% ya kifurushi, natoka one time baadae nitaweka za bolingo.

Pia jua kwamba wimbo ni umoja na nyimbo ni nyingi

Update.....

Wahenga wa Kale ifuateni post namba 24 na 26
 

Attachments

Umenikumbusha Solid Ground Family kitambo hichooo.
 
Kipindi hicho nilikua nakula kamasi bado..πŸ™πŸ™

Ila naomba unipende kama nilivyo msela ni nouma..
 
umasikini huuuu umasikin huuu enzi hizo na ndugusuluguju πŸ˜€
 
Na zote umedownload? Zinaingia kwenye folder la internal memory au memory card?
Yah,zote nime download ila inapiga hiyo moja na inajirudia hata mara 20 ,zingine sizioni kabsa,zinaingia internal,sina ext
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…