Kama wewe upo kwenye makundi haya halafu unakidharau na kukikashifu CCM tarajia laana kukuandama katika maisha yako

Ccm sio baba yako au mama yako na sio Mungu wako , pumbavu
 
Huna shukrani ww mjomba alishindwa kukusomesha ccm ikachukua jukumu lake,ccm ina upendo na inakupenda na utakuta bado ujarejesha hata senti na usumbuliwi,kuwa na shukrani
Nitaendelea kuipiga spana hadi pale itakapoacha kuwapa nafasi vilaza wawe viongozi
 
CCM daima
 
Nyerere alisomeshwa na wakoloni akawafukuza hapo vipi
 
Nyerere alisomeshwa na wakoloni akawafukuza hapo vipi
Umeshasema wakoloni,tofautisha kati ya wakoloni na chama cha mapinduzi kilichowaondoa wakoloni kikakufanya wewe kuwa huru kuwa na shukrani kwa ccm
 
Ukweli si CCM wote ni wabaya, ila mafisadi na wenye tamaa ya madaraka wengi wapo CCM. Pia sijui kwanini watu hawapendi kukosoana wakati Uhuru wa mawazo ndio huleta maendeleo.
 
ndo vile una upeo mdogo
 
Ukweli si CCM wote ni wabaya, ila mafisadi na wenye tamaa ya madaraka wengi wapo CCM. Pia sijui kwanini watu hawapendi kukosoana wakati Uhuru wa mawazo ndio huleta maendeleo.
Ni ukweli kabisa kumbuka hata shetani alitoka mbinguni,hivyo ccm watu wabaya pia wapo ila tatizo kuna watu wanajifanya vipofu ya ccm kwao haina jema hata moja,msisitizo wangu ni watu wajifunze kushukuru
 
Watanzania wamekiamini chama cha mapinduzi na chama cha mapinduzi kimeamua kuwatumikia kwa uwaminifu mkubwa,kukidharau na kukitukana ni kujitafutia laana
Nakipenda CCM,sio kwa sababu ni Chama Bora sana.
Lakini kwa kweli CCM wamefanya KAZI kubwa sana ya Maendeleo hapa Nchini.
Sina Uhakika pengine wengine wangefanya Vizuri zaidi lakini kwa bahati mbaya hawakuwahi kupata nafasi.Waliopata nafasi ni CCM na wameitendea Haki nafasi hiyo.
Nchi yetu ni Kubwa na nimebahatika kuitembelea maeneo mengi,kote huko nimekuta maendeleo.
Ukiwauliza wazee tulipotoka stori zao zitakushangaza.
Mtaani CCM inakubalika,nimeshuhudia Kwa macho yangu CCM wakipita kwa Haki kwenye Mitaa mingi Uchaguzi wa Majuzi.
Siasa za kwenye mitandao Sio halisi,watu hawayaishi Maisha ya mtandaoni..
Wananchi Wana maoni tofauti sana na hiki Chama.
Kimechokwa kwa ukongwe wake,lakini bado ni Chama Bora kinachoweza kujirekebisha,kujikosoa na kujibuni upya Kila Mara.
CCM DAIMA.
 
Laana ni nini mkuu?
 
Ubarikiwe wewe na kizazi chako,kidumu chama cha mapinduzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…