Kama Yanga haikualikwa basi ni kweli TFF ina chuki/mgogoro dhidi ya Yanga

Miongoni mwa habari ambazo zimeshtua baadhi ya wadau wa soka nchini ni habari inayohusiana na kutoalikwa kwa klabu ya Yanga katika Mkutano Mkuu wa Kawaida wa 44 wa CAF uliofanyika jijini Arusha na kufikia kilele tarehe 10 Julai, 2022.

Binafsi nimestaajabishwa si tu kwa kutoalikwa kwa klabu ya Yanga bali pia baadhi ya wadau wengine muhimu katika soka la Tanzania hasa tukizingatia kuwa Mkutano huu wa Mwaka umefanyika katika ardhi ya Tanzania.

Kwa nini nastaajabu? Ninaomba kuelezea shaka yangu kwa mujibu wa namna utaratibu wa uandaaji wa mikutano ya Kimataifa (Multilateral Conference) unavyofanyika.

Kimsingi uandaaji wa mikutano ya kimataifa kama huu wa CAF huratibiwa na pande mbili ikiwa mkutano kama huo unafanyika nje ya makao makuu ya taasisi husika.

Utaratibu upo hivi, chama cha soka/nchi mwanachama inayotaka kuomba kuandaa Mkutano Mkuu wa Mwaka itaiandikia taasisi husika (kwa muktadha huu ni CAF) kwamba inaomba kuandaa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Mwaka (Ordinary General Assembly).

Maombi rasmi yataandikwa kwa Katibu Mkuu wa taasisi kwa maandishi si chini ya miezi sita kabla ya mkutano kuanza.

Kwa mantiki hiyo TFF iliandika kuomba kuandaa Mkutano huu Mkuu wa 44 wa Kawaida wa CAF miezi sita iliyopita (labda Januari, 2022).

Kuthibitisha hilo, Rais wa TFF Warrace Karia aliweka wazi alipohojiwa na waandishi wa habari na hapa ninamnukuu;

"Mimi niliomba mkutano Serikali ikanikubalia..." Mwisho wa kunukuu.

Hivyo baada ya TFF kukubaliwa na Serikali na pia kukubaliwa na CAF taratibu za awali kuandaa mkutano (pre-meeting) zilianza.

Hapo nchi husika au chama cha soka cha nchi husika (kwa muktadha huu TFF) huandaa tarehe na eneo la kufanyika Mkutano kwa mashauriano na mamlaka husika.

Taasisi husika huandaa ajenda ya Mkutano na mlolongo (schedule) ikiwemo kanuni za mwenendo na kuzituma kwa nchi mwanachama au chama cha soka mwanachama.

Baada ya hapo kutakuwa na uratibu wa Mkutano husika.

Kikanuni, uratibu (Coordination) wa Mikutano Mikuu ya Taasisi ya Kimataifa (kama CAF) ambayo hufanyika nje ya Makao Makuu ya Taasisi hufanyika kwa usimamizi wa pande mbili yaani Nchi inayoandaa (kwa muktadha huu TFF) na Taasisi ya Kimataifa (CAF).

Kamati ya uratibu ya nchi husika iliyoandaliwa kusimamia mkutano itahusika kwa huduma zote na vifaa vyote vilivyoahidiwa na nchi inayoandaa katika barua ya maombi ya kuandaa iliyotumwa makao makuu ya taasisi na kukubaliwa na taasisi husika (CAF).

Huduma hizo zitahusisha utawala, usalama, malazi, vifaa mbalimbali, lojistiksi, usafiri n.k (Rejea OAS, 2017: 15).

Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za uandaaji wa Mikutano ya Kimataifa nchi mwanachama (kwa muktadha huu ni chama cha soka mwanachama TFF) hushirikiana na Sekretarieti ya Taasis ya Kimataifa (kwa muktadha huu ni CAF) katika uandaaji na usimamizi wa mkutano mzima kuanzia mwanzo mpaka unapofikia tamati.

Kwa mfano ukisoma muongozo wa mikutano ya OAS inaeleza hivi, 'The General Secretary will present an organization outline and it is hoped that the host country will appoint counterparts responsible for various activities.' (OAS, 2017: 16).

Hivyo basi mkutano wowote wa Kimataifa hauandaliwi na upande mmoja peke yake pale ambapo mkutano huo unafanyika nje ya makao makuu yake. Kwa mantiki hiyo TFF wameratibu mkutano huu kwa kushirikiana na CAF.

Miongoni mwa mambo muhimu yanayozingatiwa katika mikutano kama hii ni wageni wanaoalikwa.

Tukitazama mkutano wa mwaka wa 44 wa CAF tunaona kuwa mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa.

Kitendo cha kualikwa kwa Waziri Mkuu maana yake Mkutano huu ulikuwa na usalama wa hali ya juu.

Kwa mantiki hiyo hakuna mtu yeyote au taasisi yoyote ambayo ingeweza kuomba kushiriki Mkutano huu wa CAF pasina kualikwa na TFF au CAF.

Kwa mujibu wa kanuni za uandaaji wa mikutano ya Kimataifa CAF walikuwa na wajibu wa kualika viongozi wa Kimataifa huku TFF wakialika wadau mbalimbali wa Tanzania kwa kuzingatia muongozo wa uratibu wa pamoja.

Hivyo kitendo cha Yanga kutoalikwa kinatoa ishara kuwa TFF ama kwa bahati mbaya ama kwa makusudi haikuialika klabu ya Yanga jambo ambalo ni la kustaajabisha. Kwa nini ni la kustaajabisha?

Rejea maneno ya Rais wa CAF Patrice Motsepe pindi alipohojiwa na waandishi wa habari na kuambiwa 'Welcome to Tanzania' (Karibu Tanzania) hakupenda kuambiwa hivyo badala yake akawataka waseme 'Welcome home' na kuandelea kuwaambia:

"Tanzania is my home, Tanzania is his home (akimshika bega Gianni Infantino Rais wa FIFA), Tanzania is home of alla of us! Very special country! Very special history"

Rais wa CAF Patrice Motsepe anawakumbusha watanzania na dunia kuwa Tanzania si nchi ya ugenini kwake bali ni sawa na yupo nyumbani kwao Afrika Kusini kwa nini Motsepe anaamini hivi?

Motsepe aliendelea kusema:

"I'm from South Africa and the relationship between the people of Tanzania and the people of South Africa, their contribution towards our freedom...so we have got a deep deep emotional past."

Motsepe alijaribu kuwakumbusha watanzania jinsi Afrika Kusini inavyoiheshimu Tanzania na ahadi aliyoacha Mzee Nelson Mandela kuwa siku zote za maisha yao waikumbuke Tanzania na wawakumbuke watanzania.

Miongoni mwa mambo ya muhimu katika historia hii adhimu aliyotukumbushia Rais Motsepe (Rais wa CAF) ambayo labda viongozi wa TFF hawaifahamu au labda wanaifahamu lakini wameamua tu kudharau kwa utashi wao ni ushiriki wa Klabu ya Yanga katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika ikiwemo Ukombozi wa Afrika Kusini dhidi ya Walowezi wachache.

Inawezekana wachache kati ya watanzania wengi wanaotambua kuwa wakati wa harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika jengo la klabu ya Yanga lilitumika kama eneo la vikao vya siri baina ya Mwalimu Nyerere na wapigania Uhuru wa Tanganyika huku nje ya jengo hilo kundi la Taarabu la Egyptian Musical Club likitumbuiza ili kuwapumbaza wakoloni wakati ndani vikao vikiendelea (Rejea kitabu cha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Chimbuko, Misingi na Maendeleo (2022) ukurasa wa 48 mpaka 49.

Inawezekana wengi ndani ya TFF hawafahamu kuwa Yanga ndiyo klabu iliyokataa kutumiwa na vibaraka wa wakoloni ili kuzorotesha harakati za Uhuru wa Tanganyika tofauti na watani wao ambao walikubali kutumika.

Na inawezekana kabisa kuwa wengi ndani ya TFF hawafahamu kabisa kuwa Klabu ya Yanga imetambuliwa na Umoja wa Afrika (African Union) kama alama ya Urithi wa Ukombozi Afrika katika Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ijulikanayo kama "The 'Roads to Independence in Africa: The African Liberation Heritage Programme''.

Hivyo Motsepe anatambua vema umuhimu wa Tanzania katika Ukombozi wa Afrika na hivyo uwepo wa Yanga katika Mkutano huo wa CAF ulikuwa na umuhimu wa kipekee kutokana na historia ya Yanga katika harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika.

Lakini labda kama hayo yote yangekuwa hayana maana, basi labda Yanga ingealikwa kama klabu iliyobeba kombe la ligi kuu mara nyingi kuliko klabu yoyote nchini au labda ingealikwa kama klabu bingwa ya ligi kuu ya Tanzania msimu uliopita huku ikiwa imefanikiwa kunyakua makombe yote yaliyogombewa msimu wa 2021/2021.

Vinginevyo, nina shaka kama Yanga haikualikwa katika Mkutano huo wa CAF ni wazi kuwa kuna chuki/mgogoro wa TFF dhidi ya Klabu ya Yanga hasa tukizingatia utaratibu wa uandaaji wa mikutano kama hiyo na nani mwenye mamlaka ya kualika washiriki wa mkutano.

Rejea OAS (2017) Operational Handbook for the Organization of Meetings and Conferences away from Headquarters.
 
Attachments

  • Screenshot_20220812-090631.jpg
    Screenshot_20220812-090631.jpg
    94.4 KB · Views: 3

0E5091C9-C623-496A-A24C-2136CF90FF94.jpeg
 
Huo mkutano ulitangazwa sana na vyombo vya habari muda tu kuwa utafanyika Arusha. Na mikutano yote mikubwa huwa na taratibu zake hususani wanaotakiwa kuwa washiriki wa mkutano na wajumbe waalikwa na wakati mwingine hata washiriki/wasikilizaji binafsi nao hupewa taratibu za kushiriki. Iwapo viongozi wa Yanga wangekuwa makini wangeshaingia kwenye tovuti ya CAF au hata kupiga simu huko CAF kujua taratibu zipoje na wao wakitaka kushiriki wafuate taratibu zipi. Na kama wasingepata ufafanuzi mzuri basi wangewasha magari yao toka Salamander mpaka ofisi za TFF Karume kuongea na viongozi wa TFF juu kushiriki kwenye mkutano A
rusha jambo ambalo naamini kabisa wangepata maelekezo ya kutosha na huenda wangekuwa washiriki.

Kwa viongozi wa Yanga kuja kulalamika kwenye vyombo vya habari na kuilalamikia TFF tena baada ya mkutano wa CAF kwisha sidhani kama ni sahihi sana. Na pia wakati mwingine wakubali kujifunza kwa viongozi wenzao wa Simba kwani sio dhambi hasa ukizingatia mambo ya kushiriki kwenye mikutano na makongamano ya kimataifa haiathiri kabisa matokeo ya uwanjani kati ya Simba na Yanga. Babra mara nyingi tu anaonekana mitandaoni yupo CAF Cairo na juzi juzi tu hapa alikuwa Ghana kwenye mkutano mkubwa yote hiyo inamweka Babra na Simba kwa ujumla wake kwenye "platform" soka za Afrika na Dunia kwa ujumla wake.

Kwa upande wangu angekuwa amelalamika kiongozi wa zamani mzee Msola nisingeona tatizo kwani yeye ni kizazi cha "analogue" lakini malalamiko yanapotolewa na Hersi + Arafat hawa hawa wa "dot.com" napata shida kweli kweli kuwaelewa. Maana hawa wanasafiri sana nje ya nchi, wanawasiliaana na mawakala wachezaji na wachezaji wenyewe kila siku. Vipi walishindwa kuwasiliana CAF moja kwa moja kama wanaona viongozi wa TFF hawajawaalika kushiriki?

Ni matumaini yangu kuwa Hersi na Arafat watalichukulia hili suala la mkutano wa CAF uliofanyika Arusha kuwa changamoto chanya na kuwa wamejifunza kitu cha ziada kwenye uongozi wao. Bado wana mengi ya kujifunza na mengi ya kufanya vizuri kiasi cha kuthibitsha kuwa viongozi vijana wakiaminiwa kwenye soka wanaweza kufanya makubwa ya kupigiwa mfano.

Ni mtizamo tu.

Viongozi wa Yanga wame adopt ujinga wa washabiki wao oyaoya kuwaona viongozi wa TFF kuwa ni maadui wa Yanga hivyo kujenga chuki na dharau kwa TFF yote. Hapa ndiyo kauli ya msemaji wao Haji Manara kuwa ukiwa Yanga hata uwe na PhD unakuwa huna tofauti na kuli tu inapata mashiko. Sonona hii ya viongozi wa Yanga ndiyo inawafanya wanakosa ujasiri wa kushirikiana na TFF na wanaishia kulialia tu kwenye vyombo vya habari kama mtoto aliyeachishwa nyonyo na mama yake.
 
Unaalikaje timu ambayo uongozi wake hauheshimu sheria za TFF, CAF na FIFA? Fuatilia hukumu ya TFF dhidi ya Manara na kuruhusiwa kwake kushiriki siku ya Wananchi na uongozi wa Eng. Hersi! subirini tu najua mnatafuta kufungiwa maana Hatua moja huanzisha nyingine. Ambieni semaji la kimataifa Manara Bugatti liitishe Mkutano wa FIFA!
 
Shida ni Karia tu,, Usimba wake ndo unakuja kuharibu kazi ya Mpira kwa vilabu vyetu
 
Simba amechukua kombe lipi la CUF sababu mafanikio kwenye mpira ni makombe na sio kitu kingine
CUF wana makombe? Yani hata kifupi cha shirikisho la mpira Africa hujui hivi kweli wanakosea kuwaita majina mabaya kweli?
 
Shida ni Karia tu,, Usimba wake ndo unakuja kuharibu kazi ya Mpira kwa vilabu vyetu
Simba walishaalikwa Cameroon na CAF na Yanga hawakualikwa tatizo lilikua ni karia? Heb Kwa mfano sasa vile vilabu 24 vya super League vyote vipo rank ya juu Sana linganisha na Yanga. Tukubali tukatae Yanga ana Safar ndefu kimataifa na kuna level atafikia mialiko ataipata Tu hata kama karia hatak. Tusijifiche kwenye kichaka cha TFF Yanga ina hatua inatakiwa izipige
 
Laiti wangeielewa hii wangefanya ulio wajibu wao.
Hata last match agaist Simba mliifunga Simba na hamjaenda kwenye kikao cha CAF.
Tofauti ya Simba na Yanga ni kwamba Yanga inapambana kuishusha Simba wakati Simba inapambana upstairs kukuza Brand.

Kwasasa Simba kuifunga Yanga it's not a Story but Yanga kuifunga Simba it's a Story.
Jiulize.
 
CUF wana makombe? Yani hata kifupi cha shirikisho la mpira Africa hujui hivi kweli wanakosea kuwaita majina mabaya kweli?
Ile ni typing error inamaana wewe tokea uzaliwe hujawah kufanya typing error acha ujinga usipende kujikita kwenye petty issues huo ni ujinga
 
Miongoni mwa habari ambazo zimeshtua baadhi ya wadau wa soka nchini ni habari inayohusiana na kutoalikwa kwa klabu ya Yanga katika Mkutano Mkuu wa Kawaida wa 44 wa CAF uliofanyika jijini Arusha na kufikia kilele tarehe 10 Julai, 2022.
Yanga kutokualikwa sio habari ya kushtua
 
Hata last match agaist Simba mliifunga Simba na hamjaenda kwenye kikao cha CAF.
Tofauti ya Simba na Yanga ni kwamba Yanga inapambana kuishusha Simba wakati Simba inapambana upstairs kukuza Brand.

Kwasasa Simba kuifunga Yanga it's not a Story but Yanga kuifunga Simba it's a Story.
Jiulize.
Mfano makombe ya ligi kuu ya NBC yanga ana mengi kuliko Simba ni yupi anapambana kumshusha mwenzake
 
Back
Top Bottom