Kama Yanga inabebwa na waamuzi, kwanini Simba walifumua karibu kikosi kizima? Na je, waamuzi wa CAF nao wanaibeba Yanga iliyofika fainali ya CAFCC?

Kama Yanga inabebwa na waamuzi, kwanini Simba walifumua karibu kikosi kizima? Na je, waamuzi wa CAF nao wanaibeba Yanga iliyofika fainali ya CAFCC?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Tangu msimu uliopita, Simba wamekuwa wakilaumu waamuzi kuwa wanaibeba Yanga na huku Mfadhili wa Yanga, Bwana GSM akibebeswa lawama zaidi. Mbali na waamuzi, pia wamekuiwa wakiilaumu TFF kuwa inashiriki kuihujumu Simba.

Tukiacha haya ya humu nchini, wakati Yanga anafika mpaka fainali ya CAFCC, Simba walikuwa na hoja kuwa Yanga inacheza kombe la loser na wao walikuwa wanacheza ligi ya mabingwa ndio maana wao walitolewa na Yanga akaendelea mpaka fainali kwa kucheza na timu za kombe la loser.

Maswali:
Kama Simba hawakuwa na kikosi dhaifu kilichopeleke kufungwa mfululizo na Yanga na hata kutofanya vizuri kwenye ligi na kimataifa, kwanini walifumua kikosi karibu kizima cha timu yao?

Kama Yanga alikuwa anabebwa humu nchini, na waamuzi wa CAF nao walibeba Yanga mpaka kufika fainali ya kombe la shirikisho(CAFCC)?

Kwenye mechi ya marudiano hatua ya robo fainal ya kombe la CAFCL, nani aliebebwa kati ya Yanga na Mamelodi?

Hakika maswali ni mengi kuliko majibu.

All in all, kwasababu Simba hawataki kuangalia ni wapi wanakosea wajirekebishe, basi wajiandae kufungwa tena na Yanga katika mechi inayofuata na hata kufanya vibaya zaidi kwenye ligi msimu huu kuliko msimu uliopita na hata kutia aibu kwenye mashindano ya CAFCC mwaka huu.

Na wasipokuwa makini kwa kila mtu kusema hovyo hovyo, msimu huu hata nafasi ya tatu wanaweza wasiipate na wakaishia kuvurugana na itawachukua muda kurudi walipokuwa.
 
Usiangaike sana na hawa Masandakolotanouzdadi.

Kwa ufupi ndugu zetu wana timu yenye wachezaji wasioeleweka very average players.

Huwez kumtegemea mukwala mutale sijui balua akupe ushindi mbele ya Yanga yenye bacca,yao yao,boka na job.

Kwa ufupi tatizo wanalijua sema wanakosea tu namna ya kulitatua kila msimu.
 
Mbona umewauliza maswali magumu sana!

Wewe ungewauliza tu maswali mepesi kama yale zilipo bilioni 20 za mwekezaji, na sababu ya Manzoki kualikwa kuja kwenye uchaguzi mkuu wa klabu! Ndiyo watakujibu kwa urahisi.
 
Mbona umewauliza maswali magumu sana!

Wewe ungewauliza tu maswali mepesi kama yale zilipo bilioni 20 za mwekezaji, na sababu ya Manzoki kualikwa kuja kwenye uchaguzi mkuu wa klabu! Ndiyo watakujibu kwa urahisi.
Makolo hawajielewi kabisa.
 
Unauliza maswali ambayo kila siku nyinyi Chadema mmekuwa mkilalamika kuwa mnaibiwa Kula kwenye uchaguzi japo watu wanaisema Simba Ila kuna Sehemu Simba Ipo sahihi kwenye malalamiko Yao haijalishi ni Leo au kesho ila MDA utafika kila mtu atajua
 
Mzee achana na Wanasimba kwasasa, wao kwasasa ni lawama tu , hilo ni tatizo la kisaikolojia tu sio mda watanyamaza na kuona kawaida..ni kama vile kufiwa hata uambiwaje kwa faraja gani bado uchungu unakuwepo...suala la mda unanyamaza maisha yanendelea..so wanasimba watasema weee.. Ila tunawaomba wasihame ligi tu, mana itabidi tuwafate hukohuko haiwezekani tubaki peke yetu..waendelee kuitafuta furaha mbele yetu..ipo siku watafurahi na sisi tutanyamaza.
 
Viongozi wa Simba wajanja sana hizi kelele Wala hazijaja bahati mbaya walishaziandaa mapema sana na zimewasaidia na utakumbuka walishafanya hivyo mechi ya ngao ya hisani na hata sec leg litatengenezwa zengwe Moja matata
 
Sisi ndiyo Simba SC AKA;

1. Makolokolo SC.
2. Mbumbumbu SC.
3. Mipang'ang'a SC.
4. Malalamiko (Lialia) SC.
5. Makelele SC.
6. Madunduka SC.
7. Manyaunyau (mapaka) SC.
8. Mwakarobo SC.
9. Mikia SC.
10. Miso Misonda SC.
11. Manyang'au SC.
12. Mazumbukuku SC.
13. Mazombi SC.
14. Kinyume nyume SC.
15. Ngada SC.
16. Kolowizard SC
17. Zuwena SC.
18. Bebwabebwa (Mbeleko) SC.
19. Panya roads SC.
20. Kikanuni SC.
21. Kufa Kiume SC
22. Ubaya ubwege SC.
JamiiForums-312072181.jpeg
 
Watasubiri Sana kwakweli Kwa wenye jicho la mbali Simba bado Sana hijafilia kiwango cha Yanga inahitaji miaka miwili Tena..Kwa Sasa wqkubali kila aina ya matokeo.

Wale wazee waliolalama inabidi wapatie mtu wa saikolojia atakaye waambia ukweli maana Kwa hasira hizo tutarajie vifo.
 
Viongozi wa Simba wajanja sana hizi kelele Wala hazijaja bahati mbaya walishaziandaa mapema sana na zimewasaidia na utakumbuka walishafanya hivyo mechi ya ngao ya hisani na hata sec leg litatengenezwa zengwe Moja matata
Na tatizo la simba ni viongozi.Wao kazi yao nikulaumu tu wachezaji.Kama yule iliyemlaumu golikipa nilimwona hakuna kiongozi pale.Uongozi unaojielewa wa yanga ndio unaotoa matokeo na ubora wa timu uwanjani.Huwezi ukawa na uongozi wa timu mbovu alafu utegemee timu ifanye vizuri.
 
Back
Top Bottom