demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Nina taarifiwa hapa kuwa Agent wa NunguNungu amekuwa akihaha kutafuta appointment na Viongozi wa Ngazi ya juu wa yanga siku ya leo hasa Rais wa Klabu.
Kinacho msukuma kutaka kuonana na Eng Hersi Siaid ni kauli thabiti kuhusu matamanio ya mteja wake Gerard Mkude ambaye amekuwa akitamani kuweka historia ya kuvaa uzi wa #Wananchi.
Agent huyo amekuwa akipewa majibu ya hovyo na viongozi wa chini, majibu ambayo anayo dai kuwa yanamkatisha tamaa!
"Sasa nataka nizungumze na Hersi moja kwa moja maana hawa wa chini wanasema Kocha mpya ndiye mwenye kufanya mapendekezo ya kusajili, Eti wanasema nije baada Ya wiki moja na Clips za Mkude ili wamuonyeshe Kocha Gamondi l" - Alisema wakala huyo.
"Mteja wangu aligoma kuongeza mkataba kule kwa matarajio kuwa patakuwa na fursa hapa ili amalize soka lake kwa kishindo zaidi." - Aliongezea Bwana wakala.
Binafsi sioni sababu ya kwanini Mkude atamani kumaliza soka lake kwa kishindo cha mafanikio pale yanga ili hali angeweza kungoja ngoja pale Simba ili aapate fursa hiyo. Ameona nini? Mimi na wewe hatujui, huenda ana jicho la tatu ambalo sio kengeu.
Kama Hersi akimkubalia basi huenda Akavaa Medali ya CAF msimu ujao kama wenzake wallivyo fanya msimu ulio pita.