Kamachumu, Muleba: Msafara wa M/Kiti wa UVCCM Kagera waua watoto wawili

A

Anonymous

Guest
MSAFARA WA FARIS WAUWA WATOTO WAWILI KAMACHUMU MULEBA.

Msafara wa Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Biruan umewagonga na kuwauwa watoto wawili huku wengine wakijeruhiwa.

Ajali hiyo imetokea Kata Kamachumu wakati kiongozi huyo akitoka kwenye ziara yake katika wilaya ya Muleba.

Watoto hao hawajafahamika majina yao kutokana na jeshi la polisi mkoani Kagera kugoma kutoa ushirikiano kwa Waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia taarifa hiyo.

Majeruhi inasemekana wamelazwa hospital ya rufaa Bukoba.

Pia soma Mwili wa mtoto aliyegongwa na gari la Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera Faris Burhan wazikwa, simanzi kubwa yatawala kwenye familia ya mwanafunzi
 
Duh aiseee hatari
 
Si walisema magari yenye bendera ruksa kutofuata sheria za barabarani
 
Labda ndiyo ameshaanza utekelezaji wa mipango yake ya kupoteza watu.
 
Huyu dogo Faris CCM wanamlea sana inabidi awe amesimamishwa nafasi ya uongozi. Huwezi kuua na kulazimisha mtu atoke selo wakati watu ni majeruhi. Laana inamuandama ya umwagaji wa damu.
Hiki kitendo ni cha kulaaniwa kwa watanzania wote. Hizi takataka za hivi hazifai kabisa kuwa viongozi. Karma is real haya yatamrudia
 
Kwa hiyo laana yake imeua mwanafunzi asiye na hatia. Sasa kati ya mwanafunzi na yeye nani kapata adhabu?
Mawazo ya watu yanashangaza
 
Kwa hiyo laana yake imeua mwanafunzi asiye na hatia. Sasa kati ya mwanafunzi na yeye nani kapata adhabu?
Mawazo ya watu yanashangaza

Huyu kwa vile anajisikia fahari kuua, hawezi kujali, na ataendelea, mpaka siku wananchi wachukue hatua dhidi yake. Aliwaasa polisi wasifanye chochote anapoua.
 
Hii ni ajali tu kama ajali nyingine. Hakuna mahusiano ya tabia yake na ajali. Kuna waovu kupita yeye lkn hawapati ajali
 
Faris amekuwaje kwani?
Nini hasa kimempata? UVCCM wa UDOM, COED hebu niambieni huyu ndg yetu nini kimemsibu!
 
Mdomo huumba!
Alikuwa na hamu ya kumwaga damu za watu!
Sasa imemwagika ya Malaika asie na hatia!
Tuombe imwagike yake ili kuondoa laana ya mdomo wake ktk jamii Amen,
 
Chuki zako tu ,siasa za kuchafuana,acha siasa za umalaya Malaya,unaandama Hela tu hamna Lolote unapewa Vocha ukachafue watu,pole sana acha kuandama hela tafuta hela kijana hauwezi kuona mwenye hela anakuwa mtumwa saka hela kijana tofauti na apo utakuwa Mzee mchawi
 
Hilo gari la Chama Mkoa Mwenyekiti wa Jumuiya anatembeaje nalo bila Dereva wa Mkoa. ?? Kuna mambo yanasikitisha sana sana. Vijana wadogo mnavimba vichwa kwa nafasi ndogo mnazopata. Hii inaathiri hata imani ya viongozi kuwaamini vijana katika Majukum nyeti. Huyo jamaa amewatia aibu Kagera na inaonekana ana matukio mengi ya hovyo
 
Huyu ndiye Yule anaedai watu wakipotea polisi wasihangaike,anachukua pesa Kwa wakurugenzi,chama Hakuna bajeti?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…