Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
JE, WAMJUA?
Anaitwa Kamal Musatafa Atatürk (BABA WA UTURUKI)
1. Aliondosha mfumo wa Ukhalifa wa Kiislamu Khilafah ya Kiothmaniyah (Otthoman Empire) mwaka 1924.
2. Alifuta sheria zote za Kiislamu mwaka 1926.
3. Alibadilisha mfumo wa mirathi ya Kiislamu.
4. Aliwazuia Waturuki kwenda kutekeleza ibada ya Hijja na Umra.
5. Alizuia ufundishaji wa lugha ya Kiarabu Mashuleni.
6. Alizuia adhana misikitini.
7. Alizuia Hijab ndani ya Uturuki.
8. Aliondosha neno Mustafa katika jina lake.
9. Alifuta sherehe za Eid Al-Fitr na Eid Al-Adh-ha.
10. Alifanya siku ya Jumapili kuwa siku rasmi ya kupumzika badala ya Ijumaa.
11. Aliondosha matumizi ya herufi za Kiarabu katika lugha ya Kituruki.
12. Alibadilisha matumizi ya neno "Allah" katika kiapo cha uongozi.
13. Aliua mamia ya wanazuoni wa Kiislamu ambao walizikataa sera zake.
14. Kabla ya kifo chake aliusia kuwa atakapokufa watu wasimswalie swala ya Maiti kama wafanyavyo Waislamu.
15. Mwaka 1923 alisimama katika bunge la Uturuki na kusema: "Sasa tupo katika karne ya ishirini, karne ya viwanda. Hatuwezi kuendelea kufuata kitabu kinachozungumzia matunda ya Tini na Zaituni (akimaanisha Qur'an Tukufu".
Allah alimuangamiza kwa sisimizi wekundu (red ants) ambao waliutafuna mwili wake. Miaka miwili baadaye wataalamu waligundua dawa ya ugonjwa uliomuua Atatürk, na dawa hiyo inatokana na majani ya mti wa Tini uliotajwa ndani ya Qur'an.
Allah Mtukufu anasema:
"Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwishapita." (Az-Zukhruf, 43: 8)
Allah atupe mwisho mwema