Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nchi yenu isiyo kuwa na siasa kali mbona haina maendeleo?Bila huyu Uturuki ingeendelea kuwa nchi ya siasa kali na kukosa maendeleo kama Afghanistan
Hakika, japo wakina FaizaFoxy Malaria 2 Ritz na Mohamed Said wanaweza kumlaani sana.Mwamba alikuwa na akili kubwa.
Sasa mbona Uturuki ilipata maendeleo makubwa ya kiuchumi na kiviwanda kuanzia miaka ya 1999 baada ya chama cha kina Edorgan chenye mlengo wa kiisilam kuingia madarakani?Baba wa Turikiye mpya baada ya Ottoman Empire, Turkey ya viwanda, Turkey ya maendeleo makubwa kutoka kwa raia wenyewe waliofunguliwa kutoka minyororo ya tamaduni za kiimani zilizoasisiwa Mashariki ya Kati ya Waarabu
Kwahiyo kuuwa watu wenye mtazamo tofauti na ww ndo akili?
Naam, umeniita?
Nchi poa sana ile. Hakuna hata usumbufu wa adhana. Wenyewe wanajuwa muda wanakwenda kuswaliBaba wa Turikiye mpya baada ya Ottoman Empire, Turkey ya viwanda, Turkey ya maendeleo makubwa kutoka kwa raia wenyewe waliofunguliwa kutoka minyororo ya tamaduni za kiimani zilizoasisiwa Mashariki ya Kati ya Waarabu
Unapimaje maendeleo ndugu? Tanzania ni moja kati ya nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika. Unatakaje zaidi?Nchi yenu isiyo kuwa na siasa kali mbona haina maendeleo?
Ulichoandika siyo kweli. Turkey ilianza economic transformation mwaka 1930. Hiyo ya 1999 ni matokeo tu.Sasa mbona Uturuki ilipata maendeleo makubwa ya kiuchumi na kiviwanda kuanzia miaka ya 1999 baada ya chama cha kina Edorgan chenye mlengo wa kiisilam kuingia madarakani?
Wewe una weka kutunga quran?Unajuaje hana mwanzo? Unaweza vipi kuhakikisha Allah yupo na hana mwanzo, na kwamba habari hizo si hadithi za uongo za kutungwa na watu tu?
Kama nchi ambayo mpaka sasa wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati ina maendeleo basi hapa duniani hakuna nchi masikini.Unapimaje maendeleo ndugu? Tanzania ni moja kati ya nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika. Unatakaje zaidi?
View attachment 3062597 Umaskini ni wako binafsi siyo wa Taifa, acha kulialia kafanye kazi
Mbona hayo matokeo hayakutokea miaka yote mpaka yaje kutokea miaka zaidi ya 70 baada ya mapinduzi ya Atatuk?Ulichoandika siyo kweli. Turkey ilianza economic transformation mwaka 1930. Hiyo ya 1999 ni matokeo tu.
View attachment 3062598
Nikuwekee picha za homeless wa USA ndiyo utaelewa kuwa hata nchi tajiri haimaanishi kuwa watu wote wana hela na maisha mazuri kama Bill Gates, Josef Bezos au Oprah WinfreyKama nchi ambayo mpaka sasa wanafunzi wanakaa chini kwa kukosa madawati ina maendeleo basi hapa duniani hakuna nchi masikini.
Nenda kasome vizuri historia ya Uturuki naona umekaa kiudini udini tu. Hatuwezi kuelewana. Uislamu ibakie ni imani tu ya kidini kwa wananchi, kamwe usihusishe na Serikali.Mbona hayo matokeo hayakutokea miaka yote mpaka yaje kutokea miaka zaidi ya 70 baada ya mapinduzi ya Atatuk?
Mpaka miaka ya 1990 Uturuki ilikuwa taifa la ulimwengu wa tatu lakini chini ya chama cha kiislam Ak Uturuki limekuwa taifa kubwa kiuchumi ,kijeshi ,kiteknolojia.
Kiufupi nchi huwa haipati maendeleo kwa sababu ya mfumo unayo iongoza bali nchi ina pata maendeleo kwa utashi wa viongozi na wananchi wake.
Nani ambae hafi sheikh. Ufe kwa kuliwa na mdudu au presha ni yale yale cjaona uhusiano wowote wa kifo chake na ulichoandika
JE, WAMJUA?
Anaitwa Kamal Musatafa Atatürk (BABA WA UTURUKI)
1. Aliondosha mfumo wa Ukhalifa wa Kiislamu Khilafah ya Kiothmaniyah (Otthoman Empire) mwaka 1924.
2. Alifuta sheria zote za Kiislamu mwaka 1926.
3. Alibadilisha mfumo wa mirathi ya Kiislamu.
4. Aliwazuia Waturuki kwenda kutekeleza ibada ya Hijja na Umra.
5. Alizuia ufundishaji wa lugha ya Kiarabu Mashuleni.
6. Alizuia adhana misikitini.
7. Alizuia Hijab ndani ya Uturuki.
8. Aliondosha neno Mustafa katika jina lake.
9. Alifuta sherehe za Eid Al-Fitr na Eid Al-Adh-ha.
10. Alifanya siku ya Jumapili kuwa siku rasmi ya kupumzika badala ya Ijumaa.
11. Aliondosha matumizi ya herufi za Kiarabu katika lugha ya Kituruki.
12. Alibadilisha matumizi ya neno "Allah" katika kiapo cha uongozi.
13. Aliua mamia ya wanazuoni wa Kiislamu ambao walizikataa sera zake.
14. Kabla ya kifo chake aliusia kuwa atakapokufa watu wasimswalie swala ya Maiti kama wafanyavyo Waislamu.
15. Mwaka 1923 alisimama katika bunge la Uturuki na kusema: "Sasa tupo katika karne ya ishirini, karne ya viwanda. Hatuwezi kuendelea kufuata kitabu kinachozungumzia matunda ya Tini na Zaituni (akimaanisha Qur'an Tukufu".
Allah alimuangamiza kwa sisimizi wekundu (red ants) ambao waliutafuna mwili wake. Miaka miwili baadaye wataalamu waligundua dawa ya ugonjwa uliomuua Atatürk, na dawa hiyo inatokana na majani ya mti wa Tini uliotajwa ndani ya Qur'an.
Allah Mtukufu anasema:
"Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani umekwishapita." (Az-Zukhruf, 43: 8)
Allah atupe mwisho mwema
Nani kakwambia Erdogan ndio alileta maendeleo ya kiuchumi?Sasa mbona Uturuki ilipata maendeleo makubwa ya kiuchumi na kiviwanda kuanzia miaka ya 1999 baada ya chama cha kina Edorgan chenye mlengo wa kiisilam kuingia madarakani?
Utajiri wa nchi yetu uko mikononi mwa viongizi wa ccmNchi yenu isiyo kuwa na siasa kali mbona haina maendeleo?
Atatuk aliikuta Uturuki ikiwa imaya kubwa yenye nguvu ulimwenguni ,lakini mpaka ana ondoka madarakani aliacha Uturuki ikiwa imesambatika na kuifanya kijitaifa kidogo na maskini tegemezi kwa nchi za Magharibi.Nani kakwambia Erdogan ndio alileta maendeleo ya kiuchumi?
Erdogan kaikuta Uturuki ikiwa wapi, na Ataturk kaikuta Uturuki ikiwa wapi. Ataturk kaanzisha nchi, kaitoa kwenye vita, kaanzisha misingi yote ya elimu, tamaduni, viwanda, secularism na almost kila kitu. Uje umlinganishe na Erdogan ambaye Urais wenyewe kaupata kwa hisani ya Gulen.