johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam mh Mambosasa amesema tume iliyoundwa kuchunguza sakata la nyama ya wafanyabiashara imegundua nyama yote iliteketezwa.
Mambosasa amesema tume ilionyeshwa shimo kubwa ambamo minofu na mautumbo ilifukiwa na sehemu nyingine ambayo miguu na makongoro iliteketezwa kwa moto.
Hivyo siyo kweli kwamba askari waligawana nyama bali kuna kikundi cha watu wachache kilichodhamiria kulichafua jeshi la polisi amesema kamanda Mambosasa.
Kamanda Mambosasa amesisitiza kuwa bodi ya nyama ilikamata kilo 130 za nyama na wala siyo kilo 800 kama ilivyodaiwa na watu hao wenye nia mbaya na kwamba Jeshi la polisi halitawavumilia wazushi wenye nia mbaya kwa jeshi hilo.
Source: ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
www.jamiiforums.com

KASHFA: Polisi wa Buguruni Dar, wadaiwa kudhulumu kilo 800 za nyama na kugawana
Wafanyabiashara wa nyama za mafungu huko Vingunguti wamelalamikia kitendo cha Bodi ya nyama kukamata nyama zao na kuzipeleka kituo cha polisi Buguruni ambako badala ya kuiteketeza waligawana na kubakiza makongoro. Akiongea katika eneo la tukio Meya wa Jiji la Dar es Salaam mh. Kumbilamoto...