Kamanda Mambosasa: Upelelezi wa kesi ya wafuasi 27 wa CHADEMA wakiwemo viongozi wanaodaiwa kufanya fujo gereza la Segerea umekamilika

Kamanda Mambosasa: Upelelezi wa kesi ya wafuasi 27 wa CHADEMA wakiwemo viongozi wanaodaiwa kufanya fujo gereza la Segerea umekamilika

Wanasema kuwa, polisi kabla ya kufanya kazi zao kwanza, huwa wanavuta bange, na hii ni kweli.

Polisi wa Tanzania umchanie shati kwa fujo wakati yeye akiwa wapi??

Ukichelewa kutii amri yake kwa kukaa chini kwanza unapigwa rungu ama kofi.

Huu ujinga akawadanganye wajinga wenzake huko huko polisi.

Lakini wakubali kwamba walichofanya ni uhalifu na wao ni wahalifu ni majambazi na ni vibaka kama walivyo vibaka wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo ukikamatwa umeiba utasema mbona na frani kaiba!
Mwenzenu alifuata utaratibu wa mahakama.
Jibu hoja...polepole ni askari mageleza uu? Kama siyo je alikuwa kaalikwa na nani?

Nyie mnaojiita CCM mpya msituharibie nchi.
 
Rubbish statement
‪LIVE: Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM Lazaro Mambosasa anazungumza kuhusu kilichotokea juzi Segerea wakati Freeman Mbowe akisubiriwa kutoka gerezani

=====

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA


TAARIFA KWA UMMA.
KUKAMATWA KWA WAFUASI WA CHADEMA 27 KWA TUHUMA ZA KUFANYA FUJO KATIKA GEREZA LA MAHABUSU SEGEREA.

Mnamo tarehe 13.03.2020 majira ya saa 07:00 mchana Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam lilipokea taarifa kutoka kwa maofisa wa Gereza la Mahabusu Segerea kuwa kuna kundi la wafuasi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) likiongozwa na wabumbe wawili ambao ni Halima James Mdee, Ester Amos Bulaya na Meya wa Ubungo Boniface Jacob limekusanyika katika geti la kuingilia gerezani hapo huku likiandamana na kufanya fujo kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya gereza kwa lengo la kwenda kumtoa mwenyekiti wa chama chao Mhe.Freeman Mbowe.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum baada ya kupokea taarifa hizo lilituma askari wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) na askari wa kituo cha Polisi Stakishari na ambapo walipofika eneo hilo waliwakuta askari magereza wakiwa wanaendelea kuwadhibiti wanachama hao na ndipo Polisi walipowakamata watuhumiwa 27.

Baada ya watuhumiwa hao kukamatwa askari wa Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na askari wa Jeshi la magereza waliwachukua na kuwapeleka kituo cha Polisi Stakishari kwa mahojiano na baada ya mahojiano watuhumiwa wote 27 walidhaminiwa kwa mujibu wa sheria na watafikishwa mahakamani hivi karibuni kwani upelelezi wa shauri hili umeishakamilika.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo kali kwa kikundi chochote cha siasa,dini,au mtu yeyote kuacha kabisa kuchezea maeneo nyeti kama magereza,makambi ya Majeshi yote au maeneo yoyote ambayo ni nyeti kwa taifa.

Hivyo atakayejaribu kufanya hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.

WATU 03 WAPOTEZA MAISHA KWA AJARI YA BARABARANI.

Mnamo tarehe 15.03.2020 majira ya 04:30 alfajiri huko barabara ya kawawa mataa ya veta gari namba T 530 DNW aina ya EICHER daladala linalofanya safari za Mbangara- Makumbusho likitokea Mbagala kuelekea Makumbusho liligongana na gari la kubebea nyama lenye namba T 744 DET lililokuwa likitokea Tazara kuelekea katikati ya Jiji na kusababisha vifo vya watu watatu ambao ni wanaume wawili na mwanamke moja na kusababisha majeruhi ya watu nane.

Chanzo cha ajari ni daladala kutaka kuwahi kupita kwenye taa nyekundu.

LAZARO MAMBOSAS– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
15/03/2020



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkiambiwa ninyi ni POLICCM huwa hamkubali.

Hivi...kwani Mbowe hakutolewa kwa kulipiwa faini??

Kama faini ililipwa inawezekanaje watu wakamtoe Mbowe gerezani kwa nguvu??

Huyu kamanda bado hajatuambia aliyemteka Mo ni nani, anatoa longo longo tu.

Tukisema yeye anamjua aliyemteka Mo na kwamba ndiye aliyetoa amri ya kuwapiga wafuasi wa CDM na kwamba ndiye anayemuamuru kuutangazia uma ujinga huu atakataa???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii CCM Mpya na serikali yake ya awamu ya tano lazima ikemewe na kukataliwa kabisa Òktoba 2020 kupitia sanduku la kurasa.

 
March 15, 2020
Dar es Salaam, Tanzania



Leo Machi 15, 2020 Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es salaam, SACP Lazaro B. Mambosasa amezungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es salaam na kutoa taarifa ya kukamatwa kwa wanachama wa CHADEMA kwa kosa la kuleta fujo katika gereza la Segerea.
Tangu alipo sema risasi ilipigwa juu na kisha ikapinda mpaka Leo huyo simuamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu siwezi kumuamini hata kidogo.

Kwenye hiyo kesi,wanaolengwa hapo ni Mdee na Bulaya, ila haya mambo mwisho wake ni kuwafanya viongozi wa upinzani na wafuasi wao kwa ujumla kuzoe Jela na hali hii ikitimia,basi tujiandae kwa maandamano na ghasia za kisiasa haya yakiwa ni matokeo ya watu kutoogopa jela na zaidi kuwa desperate hivyo kujiona hawana cha kupoteza kukaa/kwenda jela.
Walijipeleka wenyewe!
 
Tunamuonea huyuu mambosasa anapelekeshwa na wakubwa wake roho inamuuma ila afanyaje Sasa.
Siku zote unatakiwa kusimamia ukweli, so ukikubali kuendeshwa kwa ajili ya kulinda tumbo lako ni kitu kibaya sana kwa afya ya akili yako! [emoji41][emoji41]

ˡ ˡⁱᵏᵉ ᵇⁱᵍ⁻ᵗⁱᵗᵗʸ ʷᵒᵐᵃⁿ [emoji377]
 
Pale magereza kuna kikosi kinaitwa KMGM hao FFU wanasubiri

Dk 5: Inatakiwa watu wote wanaofanya fujo wanatakiwa wawe wanaugulia nguvu ya rungu wale awapigi usoni Wanapiga kuanzia kiunoni kushuka chini

Ni kikosi maalum cha magereza Sasa wajela jela ukisikia filimbi ya hatari ya magereza unalala kama umekufa awakugusi

Lakini ukijifanya kichaa wanakuvunja kweli kiuno

Ukileta genye magereza Utajikuta mloganzila au jumba leupe la Muhimbili karibu na msikiti na kanisa kkkt..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sawa kamanda mambo sasa! Namimi nakukubari sana kamanda wangu!
Umejibu maswari yote kwa ufadaha.
Kwa ukweli
Bila chembe ya uongo.
Naamini hata mahakamani kulingana nawalichokifanya wanaenda kula mvua za ukweli ili wakirudi wakute chama kimekufa kabisa. Halima na Bulaya wanajifanya wao nividume wameenderea kufanya vitendo visivyo jadi ya watanzania sasa naona wamefika sehem wanajiona ni mwamba.
Songesha mahakamani kwa mashtaka ambayo hawaweza kuyakanusha najua hata wao watakuwa wameyaandika.
1.kwenda kumtoa mfungwa gerezani bila ridhaa ya magereza
2.kufanya funjo ndani ya eneo la magereza kwa nia ovu yakutaka wafungwa watoke.
3.kuzuia jeshi la magereza kufanya kazi zao.
Nadhani walisahau kuwa mkuu wa magereza nchini saivi ni mjeshi.
Naina miaka2 jera au faini kwa kila mmoja.
Another homo habilis pretending to be homosapiens
 
Back
Top Bottom