DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Justine Masejo, ameeleza kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu, mkoa huo umejiandaa kikamilifu zaidi kuliko wakati mwingine wowote, kwa kuwa Mkoa wa Arusha ni kivutio cha utalii hivyo kulinda usalama na amani ni mambo ya kipaumbele.
Kamanda Masejo pia amebainisha kuwa wamefanikiwa kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwa wananchi kupitia kampeni yao ya elimu katika kata mbalimbali ndani ya mkoa huo.
Ametoa kauli hiyo leo Septemba 29 2025, wakati wa mahojiano maalumu na TBC.