GE2025 Kamanda Mchunguzi: Wananchi dumisheni umoja, amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea siku ya kupiga kura

GE2025 Kamanda Mchunguzi: Wananchi dumisheni umoja, amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea siku ya kupiga kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga kuendelea kudumisha umoja, amani na utulivu katika kipindi hiki cha kuelekea siku ya kupiga kura.

Ametoa wito huo leo tarehe 21 Oktoba 2025 kupitia kipindi maalum cha TK FM Radio 88.5 Fm, akisisitiza kuwa jukumu la kulinda amani ni la kila mwananchi bila kujali nafasi au itikadi.

Kamanda Mchunguzi amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha usalama unabaki kuwa imara, huku akihimiza wananchi kuendelea kutoa taarifa mapema pale panapoonekana dalili za uvunjifu wa amani au vitendo vya uhalifu.

Screenshot 2025-10-22 233636.png
 
Back
Top Bottom