Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar Es Salaam, Jumanne Muliro, hivi karibuni akiwa anazungumza na Chief Odemba kwenye tukio maalum lililoandaliwa na TLS amezungumzia kwa uchache kuhusu sakata la kutekwa kwa Sativa.
Soma pia: Sativa: Nilitekwa na Jeshi la Polisi wakiwa na lengo la kuniua, hata nikipotea kesho Jeshi la Polisi litakuwa limehusika
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Muliro alidokeza kuwa mara ya kwanza walipomhoji Sativa, Sativa alisema kuwa alitekwa na washkaji ambao hawafahamu lakini baada ya miezi mitatu kijana huyo alibadilisha msimamo wake na kuanza kumtaja Mafwele.
"Sativa alivyopatikana alifanyiwa mahojiano na yako recorded. Alisema na wengine mlifuatilia preliminary, nilitekwa na washkaji ambao siwajui. Alitamka ni nlitekwa na washkaji ambao siwajui. Baada ya miezi 3 kupita kuna matu anajitambulisha kama whistleblower akawa anasema kwamba aliyemteka Sativa ni X na anafanya kazi ofisi Y na anavaa T shirt ya Simba na yeye ndiye aliyemchukua yule bwana"
"Baada ya pale akaibuka Sativa akapita kwenye maneno yale ya social media na kueleza jambo kama anavyolieleza"
Muliro aliongeza kwa kusema kuwa sakata la Sativa liko kwenye uchunguzi na kwamba watatoa ripoti pindi uchaguzi utakapokamilika.
Source: Mwanzo TV Plus