Kamanda Muliro adai Sativa alisema mwenyewe kuwa alitekwa na washkaji

Kamanda Muliro adai Sativa alisema mwenyewe kuwa alitekwa na washkaji

05 October 2024

SACP JUMANNE MULIRO - SISI JESHI LA POLISI NDIYO TULIMUOKOA SATIVA ALIYETEKWA JIJINI DAR ES SALAAM

Kamanda wa Polisi kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam SACP Jumanne Muliro amesema kuwa jeshi la Polisi ndilo likimuokoa Sativa aliyekuwa ametekwa kisha kuzungushwa Sehemu mbalimbali za Tanzania kisha akaokotwa Mpanda ktk pori huku akiwa na jeraha la kupigwa risasi iliyopenya kuingia ktk taya lake


View: https://m.youtube.com/watch?v=22LNIiku1W4
 
1728156677877.png

Mkazi wa Mbezi wilayani Ubungo, Edgar Mwakabela (27) almaarufu kwa jina la Sativa anayedaiwa kutoweka Juni 23, 2024.

TOKA MAKTABA :
Sativa baadaye amepatikana mkoani Rukwa nchini Tanzania baada ya kutoweka jijini Dar es Salaam Tanzania

amepatikana katika Hifaadhi ya Katavi akiwa na majeraha katika sehemu mbalimbali ya mwili wake.

Sativa ambaye alitoweka tangu Jumapili Juni 23, 2024 akiwa maeneo ya wilaya ya Ubungo jiji la Dar es Salaam .

Taarifa za kupotea kwa kijana huyo zilitolewa na familia baada ya kijana huyo kutorudi nyumbani kutoka katika fukwe maarufu za Coco beach Oysterbay jiji Dar es Salaam alikokwenda na kaka yake.


Familia ilifanya jitihada mbalimbali za kumtafuta bila mafanikio na kutoa taarifa katika kituo cha Polisi cha Kimara jijini Dar es Salaam na kupewa hati ya kipolisi ya kumbukumbu za tukio RB namba 3249/ 2024.
1728157450652.png

Picha Maktaba : Edgar Mwakabela almaarufu Sativa
 
TOKA MAKTABA :

Akizungumza na Jamhuri Digital, rafiki yake wa karibu James Nelson, amesema kuwa baada ya kusambaa kwa taarifa hizo, leo Juni 27, walipokea simu kutoka kwa wasamaria wema kuonekana kwa kijana huyo mkoani Katavi eneo Hifadhi ya Katavi akiwa amejeruhiwa nama kutelekezwa.


” Tulipata taarifa ya kuonekana kwa Sativa mkoani Katavi lakini akiwa hoi baada ya kutekwa na kupigwa na watu wasiojulikana huku miguu yake yote miwili ikiwa imevimba baada ya kupigwa” amesema.

Amesema kuwa kutokana na hali hiyo, wasamaria wema wamempeleka katika kituo cha afya cha Kibaoni kilichopo njia ya kwenda Majimoto kwa ajili ya huduma ya kwanza ya kitabibu.

“Tunawashukuru sana wasamaria wema hao na tumewaomba ndugu yetu aendelee kupata huduma zaidi wakati taratibu zingine zaidi zikiedelea.


“Hata hivyo tayari wadau mbalimbali wameanza utaratibu wa kuhakikisha Sativa anasafirishwa kwa ndege kutoka Mpanda hadi Dar es Salaam ili kupata matibabu ambapo tayari kiongozi mstaafu wa ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amechangia tiketi ya ndege
 
05 October 2024

Jaji Mstaafu Akinukisha Sakata la Utekaji na Kupotezwa Mbele ya Makamanda wa Polisi


View: https://m.youtube.com/watch?v=kyPjs32aL8E
Jaji mfawidhi mstaafu wa mahakama kuu Robert V. Makaramba atoa muhadhara mzito kuhusu watu kuchukuliwa na watu wasiojulikana nchini Tanzania na jinsi jumuiya ya kimataifa ilivyo na nguvu mtambuka bila kujali sovereignty ya nchi mambo ya utekaji yakitokea dhini ya raia zake ...

Mkataba wa agano la Rome Statue inavyowabana wanaijitetea kuwa walitekeleza amri kutoka juu ... jaji mstaafu na mhadhiri wa zamani wa chuo kikuu cha UDSM (kitivo) Law school asisitiza mapana ya sheria hizo za kimataifa na kitaifa ..
 
Hata yeye mulilo kuna watu wanamuita mshikaji haimaanishi kuitwa mshikaji kunamuondolea sifa ya kuwa Polisi🐼
Kwa maelezo ya sativa, wale madalali(washkaji) waliomtafutia nyumba ndio walimseti akamatwe..ajabu hakuna anayeongelea watu hawa..hawa walioshinikiza madalali kumpigia simu sativa waliwajulia wapi madalali kwamba wamemtafutia sativa nyumba? Kwa nini madalali hawahojiwi? ndio mambo ya watu wa kampuni za simu wnashiriki kutoa taarifa za wateja kwa polisi..hali ni ile ile km alivyokamatwa kabendera..
 
Damu ya mtu haijawahi kuacha mtu salama wameanza kujitaja code zinafunguka.
 
😂😂😂😂
Wakati wanamhoji mara ya kwanza alikuwa kwenye wenge jingi sana, Wamhoji tena sasa hivi ambapo tayari ameshapata utimamu wa akili
Kabisa, ni yale ya kumuhoji na vitisho juu ili wapate majibu wayatakayo.
 
Back
Top Bottom