Kamanda Muliro: Kuhusu stori za Mafwele naona kama riwaya za kusadikika za Shabaan Robert

Kamanda Muliro: Kuhusu stori za Mafwele naona kama riwaya za kusadikika za Shabaan Robert

tucker carlson

Senior Member
Joined
Oct 5, 2025
Posts
182
Reaction score
759
Wakati kukiwa na sintofahamu ya ukweli wa alipo Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam (ZCO), Faustine Mafwele na kile kinachozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii, Kamanda wa kanda hiyo, Jumanne Muliro ametoa kauli.

Hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii, watu waliodai kuliwakilisha kundi linalojiita Tanganyika Freedom Fighters (TFF) walichapisha ujumbe unaomuhusisha Mafwele, katika madai mbalimbali ambayo hayajathibitishwa rasmi.

Katika ujumbe huo, watu hao walitoa kauli kali dhidi ya Mafwele wakimtuhumu kwa masuala yanayohusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu.

Akifafanua sintofahamu hiyo, Kamanda Muliro ameufananisha ujumbe wa kundi hilo kama riwaya za Shabaan Robert za kusadikika. Amesema katika mambo ya kusadikika unaweza kusikia mtu amekufa halafu ukamuona.

Kamanda Muliro ametoa kauli hiyo alipoulizwa swali na mwandishi wa Mwananchi kuhusu ukweli wa ujumbe wa kundi hilo na alipo ZCO Mafwele.

Akijibu swali hilo, Kamanda Muliro alianza kwa kuelezea riwaya za Shaban Robert na kusema aliwahi kuwa na vitabu vya riwaya, moja ya vitabu hivyo ni cha kusadikika au vitu vya kufikirika.

"Kwenye jamii kuna watu na kundi la aina hiyo na katika riwaya ile (ya Shabaan Robert) alieleza moja ya majibu ya watu wenye mtazamo wa sifa za kusadikika unaweza usiwajibu, lakini majibu baadaye watayapata wenyewe.

"Mfano wanasema mtu amekufa halafu baadaye unamuona, majibu ya swali lako (kuhusu Mafwele) mimi hizo naziona kama riwaya, Shabaan Robert miaka ile alishaona hali hiyo ya kusadikika,"
amejibu Muliro.

Source: Mwananchi
 
Mnaosema Mafwele kafanyiwa abcd ndio mthibitishe. Vinginevyo ni porojo tu kama za abunuwasi.
 
Ajitokeze huyo muuaji.
Ipo siku sheria itafuata mkondo wake na nyote mlioua raia mtanyongwa.
 
Back
Top Bottom