Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

Shetani hajawahi kumshinda Mungu
Shetani hajawahi kumshinda Mungu
Kwahiyo Polisi ni Mashetani?
Una mungu wa ajabu sana wewe...

Embu kwa dakika wachana na Ushabiki wa kuchanganya dini na siasa, na UCHADEMA

Rudia tena usome nillichobandika.

Ni hivi, kama ni kweli Polisi wanadhamiria kumkamata , wanashindwa nini kumkamata halafu ndio watoe Taarifa kwamba ameitwa au kukamatwa kwa 'upotoshaji wa umma' na kwa 'lengo la kuleta taharuki' Uchonganishi wa raia na polisi?

Shetani amwingie Jakobo, umsingizie polisi. Jakobo sio Mungu wa yeyote yule.
 
Hili jeshi la Polisi ni lini liliwahi kukiri kuwa limeua raia wasio na hatia?

Walipomwua Mwangosi walisema eti ameangukiwa na kitu kizito, picha za raia ziliwaumbua kwa uwongo.

Walipowaua wafanyabiashara wa madini na kuwapora pesa zao, walidai kuwa ni majambazi na kuwa waliuawa wakati wa kurushiana risasi. Mpaka wakaenda kupiga risasi nyumba kule Sinza ili kuwahadaa watu kulikuwa na kurushiana risasi. Ushahidi wa mashuhuda na mazingira ya walikowaulia, viliwaumbua na kidhihirishia uwongo wao.

Hawa akina Muliro siyo wa kuwaamini hata kidogo:

Eti mtu agongwe na gari, afikishwe hospitali, athibitike amefariki, halafu eti ikosekane nafasi mortuary, mwili upelekwe mortuary ya polisi. Maswali ya kujiuliza;

1. Ndugu wa marehemu walikwenda vituo vyote vya polisi kuulizia habari za ndugu yao, polisi walikataa kuwa hawana habari yoyote. Mfumo wa polisi ni kwamva matukio yote ya uhalifu, ajali na yote yanayoligusa jeshi la polisi, taarifa hupelekwa vituo vyote. Kwa nini taarifa ya huyo marehemu ilifanywa tofauti na kanuni?

2. Polisi baada kuupeleka mwili wa marehemu kwenye mortuary ya polisi, hawakutoa tangazo lolote kwa umma kueleza kuwa wanashikilia mwili wa marehemu wasiyemfahamu. Tumesikia kutoka kwa ndugu wa marehemu kuwa taarifa kuwa mwili wa marehemu upo mortuary ya polisi ilitolewa kwa siri na askari mmoja. Kwa nini ilifanywa siri?
 
Kwanini hakupelekwa Temeke au Muhimbili, badala yake akapelekwa kwa mtuhumiwa?
 
Daah aisee hii taarifa sio nzuri jamaa kapotea kirahisi tu aisee harafu wanatoa taarifa kuwa aligongwa na gari wao ndio walikua wasamalia wema aisee...
 
Kitendo kilichofanywa na watu hao ni kosa kisheria na hakivumiliki na lazima Jeshi lichukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika ikiwa ni pamoja na kuwakamata , kuwahoji kwa kina na kuwafikisha mahakamani haraka iwezekanavyo.
Kwa hiyo Jeshi linamuagiza nani akawakamate?
 
Kichekesho. Mlalamikaji anataka kumkamata mtuhumiwa na kumuhoji na kumfungulia mashtaka.
 
Pale kimboka ni hatari kwa kuua wapita kwa miguu!
 
Kamanda Murilo amechemka kwa 100%. Taarifa yake imepikwa bila kuiva. Uongo wa taarifa yake uko hapa.
1. Anasema marehemu hakuwa na utambulisho wowote (yaani hata polisi walikuwa hawamju, lakini baada ya kufariki na kupelekwa hospitali ya kituo cha Polisi Kilwa, mara moja ndugu zake walifika kuuchukua mwili wake!!!

2. Polisi wanasema mwili wa marehemu ulikosa nafasi ya kuhifadhiwa hospital ya Amana hivyo wakampeleka hospitali ya kituo cha Polisi Kilwa. Hapo ndipo utata mkubwa zaidi wa taarifa ya Polisi ulipo(Tukipata muda tutajadili kwa kina).

3. Polisi wanasema wanahisi marehemu alikufa kwa kugongwa na gari, lakini hapo hapo wameshindwa kuitisha uchunguzi wa kuthibitisha kifo cha marehemu.
 
Sawa.baada ya kumchukua na kumpeleka hospital akiwa maiti je polisi walitangaza wapi kuwa kuna mtu kagongwa na gari na amefariki. Kwanini walikaa kimya?
Inawezekana Malisa na mwenzie wameingia kwenye 18. Huenda palikuwa na ajali kweli. Kama hawana ushahidi wa kukamatwa kwa marehemu na kupelekwa kituoni ambapo wanadai alipigwa basi wana kashughuli.
 
WEWE UMEFIKIRI KWA KUTUMIA BRAIN EMBEDED IN THE RECTUM

Polisi huwezi kuletewa maiti usitangaze, unakaa nayo all this time without alerting the public!
Jamaa sijui anajua kutangaza ni kutoka na kispika barabarani it's very shame
 
Ipo haja ya kuwepo siku ya hukumu kwa wanadamu wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…