Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi

Huyo muliro ameshapita Umri wa kustaafu lakini bado yupo kazini na vijana wapi mtaani hawana ajira
 
Kamanda Murilo amechemka kwa 100%. Taarifa yake imepikwa bila kuiva. Uongo wa taarifa yake uko hapa.
1. Anasema marehemu hakuwa na utambulisho wowote (yaani hata polisi walikuwa hawamju, lakini baada ya kufariki na kupelekwa hospitali ya kituo cha Polisi Kilwa, mara moja ndugu zake walifika kuuchukua mwili wake!!!
Hii inawezekana, pametokea ajali, raia wanautazama mwili, polisi wanafika wanauchukua kuufikisha hospitali, hospitali motuary zimejaa, wanapeleka kwenye sehemu yao, ndugu wanapata habari, wanaenda polisi, wanamkuta ndugu yao.

Sehemu pekee unaweza kuhisi polisi ni waongo ni iwapo:
1. Hapakuwa na ajali sehemu husika
2. Marehemu alikamatwa na polisi na kupelekwa kituoni kabla ya hiyo ajali.

Kama palikuwa kweli na ajali na marehemu hakuwa amekamatwa na polisi uwezekano kuwa polisi ni waongo ni mdogo mno.
2. Polisi wanasema mwili wa marehemu ulikosa nafasi ya kuhifadhiwa hospital ya Amana hivyo wakampeleka hospitali ya kituo cha Polisi Kilwa. Hapo ndipo utata mkubwa zaidi wa taarifa ya Polisi ulipo(Tukipata muda tutajadili kwa kina).
Inawezekana. Kama Polisi wameenda na mwili hakuna sehemu ya kuhifadhi. Wanafanyaje?
3. Polisi wanasema wanahisi marehemu alikufa kwa kugongwa na gari, lakini hapo hapo wameshindwa kuitisha uchunguzi wa kuthibitisha kifo cha marehemu.
Kwa maelezo ya polisi ni wamefika eneo la ajali wakamkuta na kuna watu wengi hilo eneo walioshuhudia hiyo ajali, wao wakaondoka na mwili.
 
Kupotosha na kugombanisha serikali kwa wananchi ili waichukie kwa kuandika habari za uongo sasa umeyatimba, Kamanda Muliro amekuita pale central akachukue maelezo yako na akupumzishe angalau wiki ili upunguze uzito uliokuwa nao maana kila ukishauriwa na Prof Janab hutaki, sasa Muliro atakusaidia kupungua mwili.

Kule unakwenda kukutana na wanaume haswa pale mahabusu, wakikuuliza umefuata nini waambie ulifanya jambo la hatari, usije kuwaambia masela mahabusu kuwa umekamatwa kwa kosa la uzushi, aisee utatoka vibaya huko mahabusu.
Leo nzima nasikia unamsumbua Kibatala akakusaidie, mnatukana na kuzusha halafu yakiwakuta mnaanza kulia kulia.

Kamanda Muliro nakuom sana huyo jamaa mdake ijumaa akae humo had j3, shenzi kabisa
 
Hii kesi tamu sana.

Polisi wakienda mahakamani watajivua nguo sana.

Yaani Mortuary ilijaa, then wakaona ni vyema kuhamishia Maiti Mortuary ya Kituo cha Afya cha Polisi. Hapa ni step ya kwanza kubugi kwenye movie yao.
 
Kupotosha na kugombanisha serikali kwa wananchi ili waichukie kwa kuandika habari za uongo sasa umeyatimba, Kamanda Muliro amekuita pale central akachukue maelezo yako na akupumzishe angalau wiki ili upunguze uzito uliokuwa nao maana kila ukishauriwa na Prof Janab hutaki, sasa Muliro atakusaidia kupungua mwili.

Kule unakwenda kukutana na wanaume haswa pale mahabusu, wakikuuliza umefuata nini waambie ulifanya jambo la hatari, usije kuwaambia masela mahabusu kuwa umekamatwa kwa kosa la uzushi, aisee utatoka vibaya huko mahabusu.
Leo nzima nasikia unamsumbua Kibatala akakusaidie, mnatukana na kuzusha halafu yakiwakuta mnaanza kulia kulia.

Kamanda Muliro nakuom sana huyo jamaa mdake ijumaa akae humo had j3, shenzi kabisa

Nina wasi wasi kama wewe ni mwanaume.
 
Haya maelezo ya Kamanda yanafikirisha sana..
 
Mleta mada eti ni mwanaume Yaani midudu kama hii ndo imo kwenye mfumo mwekezaji akija anabeba Mali anaondoka anatuachia madeni na mijitu IPO inapumua kote kote mdomoni na kule kwingine kuisubir chadema lakini mwekezaji anakwiba Mali mchana kweupeee kazi yao ni kusimamia wapiga sahihi wapige sahihi wao wanaambulia per diem na supu ya mapupu asubuhi kazi ni majungu tu kama hili dude lilileta hii mada
 
Kunapokuwa na vacuum uchafu unaweza kuingia.
Ni muhimu kutoa taarifa sahihi kwa wakati sahihi kunapokuwa na jambo lisiloeleweka, hasa linalohusu usalama wa raia (uhai/maisha).
Kama walipotosha baada ya taarifa sahihi kutolewa hapo kuna uzito, vinginevyo wapewe onyo na maelekezo ya kutulia, kutumia akili na busara kabla ya kueneza taarifa inayoweza kusababisha taharuki.
 
Hata kama ni kweli, yaani Jeshi la Polisi limeokotoka mtu amegongwa na akafariki, Mtanzania makini hawezi kuamini chombo hiki maana kilishajitoa kwenye orodha ya kuaminika. Jeshi la Polisi ni chombo kisicho aminika hapa Tanzania kuliko taasisi zote.
 
siku zote huwa kamanda anatoa taarifa mbalimbali za matukio mbona hili kaka kimya na Je iweje mtu atolewe amana apelekwe hospitali ya polisi yaan utoke ilala uende temeke wakati kuna Muhimbili?
na Pia kwa nini polisi kule.mochwari yao wanasema aliletwa na polisi akatelekezwa hapo! hili suala litamfukuzisha hapo!
Kamanda' soon atakuja kusema mochwari ya muhimbili ilikuwa imejaa😭
 
Ukiona hivyo ujua CCM wamesha anza kutoa maagizo. Rais alisema kila kiongozi kwenye eneo lake ajifunze na kufuata-4-R. Sasa Murilo kaanza kukamata,Kuhiji kwa kina SANA, na kufikisha Mahakamani HARAKA?
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ya uongo na uzushi inayosambaa katika mitandao ya kijamii kuhusiana na kifo cha Robart Mushi @ Babu G. ambaye picha yake imeambatanishwa kwenye taarifa hizo kuwa alipotea tarehe 11 Aprili, 2024 na baadae kugundulika katika Chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Polisi Kilwa Road huku ikidaiwa Polisi kuhusika na kifo hicho kwa kumuua..

Ukweli ni kwamba tarehe 11 Aprili, 2024 majira ya saa 10 Alfajiri Askari Polisi wa Usalama barabarani alipewa taarifa na mwananchi kuwa eneo laTaa za kuongozea magari za Buguruni, Ilala mtu mmoja mwanaume aliyekuwa akivuka barabara eneo hilo la Kimboka kuelekea Chama aligongwa na gari ambalo halikusimama (hit and Run).

Mtu huyo alipata majeraha makubwa kichwani, kifuani na eneo la chini la mgongo na kisigino cha mguu wa kulia. Eneo hilo lina watu wengi ambao wanakesha kwa biashara mbalimbali na walishuhudia tukio hilo.

Mtu huyo alipelekwa haraka hospitali ya Amana na Polisi lakini baada ya kumfikisha Madaktari walibaini kuwa mtu huyo alikuwa tayari amekwishafariki, Kwa sababu chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Amana kilikuwa hakina nafasi, ilishauriwa akahifadhiwe kwenye Hospitali ya Jeshi la Polisi iliyo barabara ya Kilwa Temeke ambayo inatoa huduma hata kwa raia kuhusiana na suala hilo.Tarehe 21.4,2024 ndugu wa marehemu walipatikana na wakautambua mwili wa ndugu yao kwani hakuwa na kitambulisho wala simu. Taratibu za mwisho za mazishi zinafanywa ili akazikwe.

Kutokana na taharuki iliyotengenezwa na kujengwa kwa makusudi na mtu anayejiita Malisa gj na Bonoface Jacob ambao kwenye “post” zao walionesha nia ya wazi ya kutengeneza chuki dhidi ya Polisi na Serikali kwa wananchi kuwa mtu huyo aliyepata ajali alikuwa ameuawa na Polisi , Kitendo kilichofanywa na watu hao ni kosa kisheria na hakivumiliki na lazima Jeshi lichukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika ikiwa ni pamoja na kuwakamata , kuwahoji kwa kina na kuwafikisha mahakamani haraka iwezekanavyo.

Jeshi la Polisi halitavumilia watu ambao wanaibuka na taarifa za uongo na uzushi ambazo zinalenga kujenga chuki na taharuki kwa wananchi. Jeshi litaendelea kusimamia misingi ya kisheria na halitakuwa na huruma kwa mtuhumiwa yoyote wa kihalifu na litamshughulikia haraka iwezekanavyo kwa mujibu wa sheria.

Imetolewa na ;
Muliro J. MULIRO - SACP
Kamanda wa Polisi
Kanda Maalum ya Dar es Salaam

Pia soma:


Mauaji ya Robert Mushi ndugu wa aliyekuwa Meya wa Ubungo Boniface Jacob polisi wanahusika?
""WAKAMATWE NA WAFUNGULIWE MASHTAKA, ILI IWE FUNZO KWA WENGINE KUONGEA NA KUPINDISHA UKWELI HALISIA WA JAMBO LOLOTE LILE""
 
Mmmm taarifa imepikwaaas......haswaaaa
Nenda Buguruni, pale kuna watu hawalali usiku na wanabiashara zao waulize utapata jawabu, Imefikia pahala watanzania lazima wawe wakweli, hao jamaa washughulikiwe kikamilifu kwa upotoshaji.
 
Muliro hajasema kama jeshi la polisi baada ya kupata taarifa ya marehemu kugongwa na gari, nao kufika kuuchukua mwili na kuupeleka mochwari, walitoa taarifa yoyote juu ya hilo tukio kwa umma?

Nijuavyo, kawaida kwenye matukio kama hayo, polisi huwa wana kawaida ya kutoa ripoti za kiusalama kwa raia, kama hilo tukio la ajali pia walitakiwa kutoa taarifa yake, lakini mbona wakanyamaza kimya mpaka ndugu wa marehemu wahangaike kwa siku kadhaa kumtafuta ndugu yao?

Jeshi la polisi ili lionekane linafanya kazi zake kwa weledi, kwanza lazima litoke kwenye hii mindset ya kutishana lihamie kwenye mindset ya kuelekezana, wawe wanajibu maswali ya msingi ili kuondoa sintofahamu zisizo na maana kwa raia wake, watengeneze mazingira ya kirafiki na jamii ili iwe rahisi kwao kupewa taarifa za kiusalama kila wakati.

Vinginevyo wataendelea kuonekana wababe waogopwe na raia, tuendelee kuishi kama paka na panya siku zote.
Wamekosa professionalism imagine huyo ndio Boss wao wa mkoa je wale polisi wa chini kabisa watakuwaje?
 
Kama watakamatwa,wanahitajlka mawakili nguli wa kuwatetea!
 
Back
Top Bottom