Kamanda Muliro: Ndio maana sitaki kubishana, Jeshi la Polisi ndio lilimuokoa Sativa kule Katavi!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Mnakumbuka ile clip ya Sativa baada ya kupatikana kule Katavi na akiwa amezungukwa na wananchi ambao ndio walijitolea kumpeleka hospitali na kuhakikisha anakutana tena na familia yake?

Kama utakuwa hujaona hiyo clip, nimeiweka hapo chini.

Ni clip inayomuonesha Sativa akiwa amezingirwa na wananchi ambao ndio walimpeleka hospitali kupata matibabu.

Soma pia: SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Oysterbay kabla ya kusafirishwa sehemu nyingine na nimepigwa risasi ya kichwa

Sasa leo wakati anazungumza na Chief Odemba, Kamanda Muliro amesema kuwa Jeshi La Polisi ndio lilimuokoa Sativa baada ya kukamatwa na wasiojulikana. Muliro alidokeza kuwa Jeshi La Polisi ndio lilihusika katika kumuokoa Sativa pindi alipotekwa.

"Sisi ndio tulimuokoa (Sativa) ndio maana sitaki kubishana. Sisi ndio tulimuokoa kule Katavi tukampeleka kituo cha Polisi. Sisi jukumu letu baada ya taarifa ile, tulimuokoa muhusika yule. Sasa kama unataka au hautaki sisi ndo tulimuokoa muhusika yule"

Ningependa kumaliza uzi wangu kwa kukumbusha maneno mazuri ya lugha kuwa "Ogopa sana Mungu na Teknolojia" maana kusingekuwa na hii clip leo taifa lote tungelishwa tango pori.

Nawasilisha!

Your browser is not able to display this video.


Your browser is not able to display this video.
 
Yawezekana hao unaowaita wananchi ni askari polisi ktk nguo za kiraia.
 
Damu za watu zimeanza kumlilia....hapo ni kama akili zimefyatuka hivi...
 
Hao wanaomuuliza hapo siyo raia kabisa. Hao ni polisi na ndiyo waiomuokoa.

Msidanganye watu.
 
Reactions: Lax
Ni kweli kabsa Polisi waliokoa maisha ya Sativa ila unajua iliokoaje maisha ya Sativa!?

Ilimuokoa kwa kushindwa kumpiga risasi ya kichwa na wakampiga risasi ya taya. Hapo ndo walipofanya kumuokoa Sativa.

Ila kama kweli anaweza kuongea kwa jeuri hivi, ipo siku atapata taarifa kuwa kijana wake amepigwa risasi ndo atafahamu uchungu wa kuropoka maneno haya.
 
Kwani we umejuaje kuwa hao siyo maafande,msipende kubishabisha vitu msivyovijua
Mbona maswali yako yamekaa kimtego eti "umejuaje" !. Hilo lililo simama hapo nyuma ni gari la police? hao wanao mhoji ni mapolice ?
 
Hana mshipa wa aibu mtu mzima muongo kwasababu ya kulinda cheo
 
Mlimuokoaje SATIVA wakati polisi ndiyo walimpeleka Karakana ya o6bay kisha kituo cha polisi arusha then polisi hao hao wakampeleka Katavi wakampa chuma kikapita pembeni ya mshipa medula kikafumua taya? na kumuacha pembeni ya mto wenye mamba na viboko na sehemu ya wanyama wakali kama simba tembo chui wanapokunywa maji? Utasemaje ndiyo mliomuokoa?
 
Sativa laZima atamjibu 😄
Ligi imeanza upya

Ova
 
Kumbe katika polisi kuna kitengo cha UTEKAJI na kitengo cha uokoaji.
Safi sana.
Na pale oyster Bay kuna kitengo gani?
Mafundi gereji?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…