Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Mnakumbuka ile clip ya Sativa baada ya kupatikana kule Katavi na akiwa amezungukwa na wananchi ambao ndio walijitolea kumpeleka hospitali na kuhakikisha anakutana tena na familia yake?
Kama utakuwa hujaona hiyo clip, nimeiweka hapo chini.
Ni clip inayomuonesha Sativa akiwa amezingirwa na wananchi ambao ndio walimpeleka hospitali kupata matibabu.
Soma pia: SATIVA: Nilitekwa nikapelekwa Karakana ya Polisi Oysterbay kabla ya kusafirishwa sehemu nyingine na nimepigwa risasi ya kichwa
Sasa leo wakati anazungumza na Chief Odemba, Kamanda Muliro amesema kuwa Jeshi La Polisi ndio lilimuokoa Sativa baada ya kukamatwa na wasiojulikana. Muliro alidokeza kuwa Jeshi La Polisi ndio lilihusika katika kumuokoa Sativa pindi alipotekwa.
"Sisi ndio tulimuokoa (Sativa) ndio maana sitaki kubishana. Sisi ndio tulimuokoa kule Katavi tukampeleka kituo cha Polisi. Sisi jukumu letu baada ya taarifa ile, tulimuokoa muhusika yule. Sasa kama unataka au hautaki sisi ndo tulimuokoa muhusika yule"
Ningependa kumaliza uzi wangu kwa kukumbusha maneno mazuri ya lugha kuwa "Ogopa sana Mungu na Teknolojia" maana kusingekuwa na hii clip leo taifa lote tungelishwa tango pori.
Nawasilisha!