Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Kamanda Jumanne Muliro, tuache unafiki, tuache kuoneana. Unatutangazia kuwasimamisha hawa Polisi wawili walioonekana wakichukua fedha kwa makondakta wa dadadala kwa sababu wamefanya kosa au kwa sababu wameanikwa mitandaoni?
Ina maana hujui kwamba kila siku traffic wanaokuwa barabarani wanafanya hivyo? Leo ndio unajua?
Yaani unataka kutuambia hujui kwamba hata wakuu wao wa vituo, wanapowapeleka barabarani, wakirudi jioni wanawadai mgao wao? Hujui kwamba wasipopeleka mgao hawatawekwa tena barabarani? Unafikiri hela walizokuwa wakichukua ni zao peke yao? Kama hujui hili hufai hata kuwa na nafasi uliyonayo!
Acha kuonea watu kwa kujaribu kuficha aibu. Ni jambo linalojulikana na kila mtu kwamba polisi wakiwa barabarani wanatakiwa kurudi ofisini na mgao wa wakuu wao. Unafikiri wanaupata wapi?
Na sio traffic tu, hata wale askari wanaopangiwa kufanya patrol, iwe usiku au mchana, wakirudi ofisini wanatakiwa wapeleke mgao kwa wakuu wao, la sivyo hawapangwi kwenye detail za patrol. Kupewa ile SMG kwenda Patrol maana yake unapewa jukumu la kurudi na mgao wa afande wako. Hilolinajulikana na kila askari.
Sasa usijikoshe kinafiki kwa kusema jeshi la Polisi limechafuliwa. Jeshi la Polisi ni chafu tu tunajua, na huwezi kujikosha mbele ya umma kwa kulisafisha kwa kuwasimamisha hawa wawili. Walichofanya ni jambo la kawaida ndani ya polisi na hata wewe unajua ndivyo ilivyo.
Polisi yeyote alie barabarani anatakiwa apate chochote kutoka daladala, gari za mizigo (kenta) na gari za mchanga. Hakuna gari kenta au ya mchanga itafanya kazi bila kutoa mgao kwa polisi hata siku moja, na hao polisi walio barabarani wakuu wao wanawapangia kabisa fungu la kuwapelekea.
Hata hivyo, Magufuli si aliwaruhusu madereva wawape hela ya ku-brashia viatu? Na Samia si amesema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake? Sasa unafikiri urefu wa kamba ya polisi ni mshahara peke yake? Umemuuliza Samia alimaanisha nin Polisi kula kwa urefu wa kamba yao?
Hebu warudishe kazini hawa askari wawili. Acha uonevu na kujikomba kwa watu, ni unafiki tu unaofanya hapo. Si ajabu hata wewe mwenyewe Muliro unaletewa magao wako, usitudanganye hapa.