Kamanda Siro: Wema Sepetu, TID na Nyandu Tozi bado wanashikiliwa na jeshi la polisi

Kamanda Siro: Wema Sepetu, TID na Nyandu Tozi bado wanashikiliwa na jeshi la polisi

brave one

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
4,879
Reaction score
7,386
Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa
kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi hilo.

“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,”amesema Sirro kwa kifupi. Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.

Source: mwananchi

=======
Wema Sepetu kukamatwa na kuhukumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya
Yaliyojiri katikati ya mchakato wa upelelezi wa kesi ya wema
Wema kukutwa na kesi ya kujibu
Kuhukumiwa na kuachiwa huru baada ya kulipa faini
 
Maskini hadi huruma. Kama wanatumia kweli hayo madawa watalegea sana. Hapo kutoka mpaka jumatatu. (Boss wema application yetu updates ndio mpaka jnne,maana jumatatu atatoka na hasira mpaka zipungue)
 
So na leo kalala huko?
 
HAIDARY KAVILA NDIO YULE BWANA MDOGO ANAYETEMBELEA MAGARI YA KIFAHARI?
 
Mbona maaskari hawaongelewi siyo watu au? Nchi hii inatukuza sana wasanii ndo maana wanaharibikiwa!
 
Naona dalili ya watu kulipwa fidia ya mamilioni kwa kukashifiwa..
 
Hawa ni watumiaji au wauzaji?
Mtumiaji.na.muuzaji wote sawa tatu maana hakuna muuzaji bila mtumiaji. Wote wakamatwe tu. Nashauri wawachukue vipimo vya damu na ikithibitika washitakiwe kwa kutaka kujidhuru na wakati wanajua.
 
Back
Top Bottom