Kamanda wa CHADEMA akinukisha Gold FM, Kahama

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kwa hakika CHADEMA imekamilika. Kwa maana makamanda wake takribani wote, ni moto πŸ’₯πŸ”₯πŸ’₯!

Your browser is not able to play this audio.


Akihojiwa live leo na kituo hicho maarufu 88.7 pande za huko, kamanda huyo hakumung'unya maneno.

"Kwamba:

1. Bila katiba mpya, kwa hali ya sasa rais anaweza kufanya lolote ikiwamo ndivyo sivyo bila kuwajibika kokote. Kuwa anaweza hata kuamua kutulaza vyooni.

2. Amesisitiza hakipo cha kumpongeza rais kwa kuruhusu mikutano wala maandamano kwani hayapo leo kwa hisani yake.

3. Akieleza zaidi, amesisitiza hata ushirikiano mgeni huu tunauona leo na polisi kwenye shughuli za siasa, siyo hisani."


Amesema mengi kamanda huyo yenye hamasa kubwa kuonyesha kesho bora ya nchi hii ikiwamo hali hohehahe mno ya barabara za manispaa hiyo chini ya ma CCM.

Kwa hakika kanda ya ziwa, kina "ngosha" wako tayari.

 
Kazi ya ukombozi inaendelea
 
Nchi tulokuwa tunataka hii Hapa.

Watangazaji unaona kabisa wanajisikia Amani kuongea na wawakilishi wa vyama
 
fanya kazi acha kuropoka hovyo kijana hali ngumu ya maisha unaitaka mwenyewe kukaa vijiweni bila kufanya kazi
 
Nchi tulokuwa tunataka hii Hapa.

Watangazaji unaona kabisa wanajisikia Amani kuongea na wawakilishi wa vyama

Naambiwa hiyo radio ni mali binafsi ya mbunge (CCM) wa huko.

Sikuweza kuinukuu yote ila ilikuwa interview ya over 30min πŸ’₯πŸ”₯πŸ’₯πŸ’₯
 
Mwandishi atumie akili, eti Rais kasaidia maandamano. Rais kufanya hivyo ni kaonyesha udhaifu wake
 
Mwandishi atumie akili, eti Rais kasaidia maandamano. Rais kufanya hivyo ni kaonyesha udhaifu wake
Radio mali ya ya mbunge CCM. Tajiri hapo ni mboga mboga nguli. Kurusha interview kama ilivyokuwa live nadhani wanastahili pongezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…