GE2025 Kamanda wa Polisi Tanga: Anayefikiri kuweza kuvunja amani asijidanganye na asijaribu, Tutawashughulikia

GE2025 Kamanda wa Polisi Tanga: Anayefikiri kuweza kuvunja amani asijidanganye na asijaribu, Tutawashughulikia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi, amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Tanga kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 29 Oktoba 2025, akibainisha kuwa hakuna tishio lolote la amani lililopo kwa sasa

Akizungumza Oktoba 18 2025, akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Kamati ya Amani na viongozi wa kisiasa, ACP Mchunguzi amesema Jeshi la Polisi limejipanga kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuwepo kabla, wakati na baada ya uchaguzi

Amesema baadhi ya watu wanaohamasisha uvunjifu wa amani tayari wamekamatwa kwa mahojiano, na endapo watabainika na makosa watafikishwa kwenye vyombo vya sheria

Kamanda Mchunguzi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa mapema pale panapoonekana dalili za uchochezi, na kuhakikisha Tanga inabaki kuwa mfano wa amani na utulivu nchini

Soma pia GE2025 - Kamati ya Ulinzi na Usalama Tanga yatoa onyo kwa watakaovuruga Amani siku ya Uchaguzi

 
Huu Uchaguzi Mpaka Sasa Vyombo Vya Habari Vimeandika Na Kutoa Taarifa Nying Kwa Vyombo Vya Usalama Na Ulinzi Waraia

Kuliko Kutoa Taarifa Kwa Wananchi Kuhusu Uchaguz Wao Ndiyo Wahusika Wakuu Inashangaza
 
Matamko yamekuwa ni mengi mpaka inashangaza! Hofu kwa wahuni imetanda kila mahali.
Mbona we comments za kupiga mikwara mitandaoni kuwa utaandamana zimekua nyingi kuliko vitendo?
 
Yaani wanavyozidi kuwatishia ndipo wanaharibu zaidi.
 
MaRpc, Rc na maDc kazi wanayo kipindi hiki cha uchaguzi, matamko yanatiririka kama aji. Kwa sasa nadhani usiku wakilala wanaota kwa sauti "Ole wake atakae hamasisha uvunjifu wa amani atakiona cha mtema kuni" adi wanastuliwa na weza wao kuwa wapo kitandani wamelala. Uchaguzi wa mwaka huu unawapa tabu sana.
 
Ni wezi, mafisadi, waroho, wabinafsi, watekaji, wauaji, wanyanyasaji, wanaoogopesha watu Ili waendelee na maovu yao!
Watakoma mwaka huu!
 
Back
Top Bottom