Kamanda wa uasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati akamatwa na ICC

Kamanda wa uasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati akamatwa na ICC

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mahakama ya kimataifa ya jinai ya ICC, Jumapili imesema kuwa imemtia mbaroni aliyekuwa kamanda wa kundi la uasi la Seleka huko Jamhuri ya Afrika ya Kati linaloshukiwa kutekeleza juhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, ICC imesema kuwa Mahamat Said Abdel Kain alijisalimisha Jumapili na kukamatwa kufuatia hati ya iliotolewa Januari 7, 2019 kutokana ukatili uliotekelezwa 2013.

Hata hivyo tarehe ya kufikishwa mbele ya mahakama mjini Hague haijatangazwa. Ukamataji huo umefanyika wakati kukiwa na hali ya taharuki nchini humo kufuatia mapigano kati ya jeshi la serikali likiungwa mkono na Russia na Rwanda na waasi wanaopinga ushindi wa rais Faustin Archange Touadera kufuatia uchaguzi wa Decemba 27.

Taifa hilo limekuwa likishuhudia machafuko tangu muungano wa waasi wa kiislamu kutoka upande wa kaskazini kwa jina Seleka walipochukua madaraka Machi 2013. Utawala wao ulipekea wapiganaji wa kikristo kwa jina anti balaka ambao wengi wa viongozi wao wanakabiliwa na mashihtaka mbele ya ICC.

1611549563064.png
 
Vitu kama hivi Sweden, Norway, Denmark, Finland havipo, why on Africa, Black men?
 
Vitu kama hivi Sweden , Norway, Denmark, Finland havipo, why on Africa, Black men?
Vinatokana na roho kama zenu kupinga kila kitu bila ideology. Tueleze Tundu Lissu ana ideology ipi sana sana ni JPM aondoke madarakani ili naye afaidi ikulu. Ubinafsi ukizidi ndiyo matokeo yake.

Wewe mwenyewe hakuna hata moja ambalo JPM amelifanya ukalikubali. Kila siku kupinga tu
 
Well Said
 
Back
Top Bottom