Kamara Kusupa: Rais amepata wa kuendana naye. Je, ataacha kulalama?

Ila kweli huyu bwana mdogo amerushwa mno.

hata kama ni urafiki siyo hivyo, unamtoa paramagamba unamuingiza dogo ambaye ni mwororo kabisa kwenye siasa.

Angemweka hata jon mnyika au zito zuberi kabwe.

kwani upinzani nchi ni dhambi?
 
Hapo kwenye umeme kajichimbia kaburi lake
 
Criterion!
Hongera sana, umenyoosha maneno bila chenga.
 
Kikubwa nilichokuelewa hapa ni usikivu, you mean Father of Nation alikuwa Msikivu.
 
Rais Samia amewastaajabisha Watanzania makini alipofika New York alikuwa na wakati mzuri na Bi. Mange Kimambi “mtukanaji” anayejulikana wazi alivyoisemea mbovu serikali ya Magufuli.
Duh!....
 
Baadaye nilisikia jinsi Rais Biden wa Marekani alivyoutolea nje ujumbe wa Tanzania, hakukutana na Rais wetu hata kwa mazungumzo ya salamu tu za dakika chache. Rais Biden hakutaka hata kupiga picha ya pamoja na Rais Samia!
Rais alienda kwenye mkutano wa UN na sio ziara ya kikazi huko US hivyo hilo la kukutana na Biden halikuwa malengo ya ziara hivyo hakukuwa na ulazima labda Biden mwenyewe angetaka..... isitoshe sio kila kiongozi wa nchi aliyekuwepo huko New York alikutana na Biden.

Yawezekana Biden alijiepusha na “demonize” yaani picha moja aonekane yuko na Rais wa nchi, kisha picha nyingine huyo Rais aliyeonana na Biden, anaonekana yuko na “vimange?” Hapana! Hilo lingeifedhehesha Marekani kama dola.
Huu ni mtazamo wako binafsi...
 
Kila anapoapishwa rais mbele ya jaji mkuu huwa inaanza awamu mpya. Anaingia madarakani akiwa na wasaidizi wote wapya kila kitu huanza upya kabisa.

Ni vigumu mno maadui wa JPM wakawa ni maadui wa Samia. Ni ngumu kwa marafiki wa JPM wakawa ni wa Samia. Kila nafsi imeumbwa tofauti na nyingine na pengine ni kwa masuala mengi ya kiutendaji.

Wanachokosea wengi ni kumfananisha Samia na JPM hata kama kisiasa aliwahi kusema yeye na JPM ni kitu kimoja. Hawa ni nafsi mbili tofauti zenye fikra, ujasiri na uzalendo wenye kutofautiana.
 
Hakuna mbunge halali pale hata mmoja

Wote ni wezi wa kura na matapeli walishiriki kunajis uchaguzi 2020.

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…